MASELE AMPONGEZA MAMA SAMIA KWA KUTIMIZA MIAKA MIWILI YA UONGOZI THABITIAliyekuwa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika(PAP) na Mbunge mstaafu wa Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili tangu achukue madaraka kutoka kwa mtangulizi wake Hayati Dkt.  John Pombe Magufuli.

 Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Masele amesema Rais Samia amekuwa Rais bora, mtulivu na mwenye busara na Hekima wakati wote anapofanya maamuzi ya nchi. Ameliongoza taifa kwa kujenga umoja wa kitaifa na kuweka mbele maslahi ya taifa mbele.

Mhe. Masele amemtakia Rais Samia afya njema , furaha na maisha marefu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post