MIKUTANO YA KAMATI ZA BUNGE LA AFRIKA (PAP) NA VYOMBO VINGINE VYA PAP YAANZA KUUNGURUMA

Rais wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament (PAP), Mhe. Chifu Fortune Charumbira akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mikutano ya Kamati za Kudumu za Bunge la Afrika (PAP) na vyombo vingine vya Bunge Afrika itakayofanyika kuanzia Machi 6, 2023 hadi Machi 17,2023 katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini vikiongozwa na Kaulimbiu ya Umoja wa Afrika (AU) ya 2023 "Mwaka wa AfCFTA: Kuharakisha Utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika".


Sherehe hizo za ufunguzi zilizofanyika Jumatatu Machi 6,2023 zimehudhuriwa pia na wageni wa ngazi za juu akiwemo Mhe. Candice Mashego-Dlamini, Naibu Waziri wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa.


Akizungumza, Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Chifu Fortune Charumbira amesema Kamati za Kudumu ndizo waendeshaji wakuu katika kutoa matarajio ya raia wa Afrika hivyo kuziagiza Kamati hizo kueleza kikamilifu matarajio ya watu wa Afrika .


"Ili Kamati zetu ziweze kuchangia katika kurekebisha masuala yanayoikabili Afrika, tunapaswa kuwa wazi juu ya orodha kamili ya masuala ambayo yanaathiri vibaya watu wetu. Ni lazima, kwa hiyo, kutumia vikao hivi kufanya uchunguzi wa mazingira kwa hadubini, kuandaa orodha ya kina ya changamoto zinazowakabili wananchi wetu na kuandaa mipango kazi ambayo inatoa kipaumbele na kukabiliana na masuala yaliyoainishwa. Mtazamo wetu lazima ubaki thabiti juu ya mahitaji na matarajio ya raia wa Afrika na hapo ndipo tunaweza kusalia kuwa muhimu kama taasisi ya uangalizi na uwakilishi wa bara," amesema Chifu Charumbira.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post