WALENGWA WA TASAF WAHIMIZWA KUCHANGIA ASILIMIA 10 YA NGUVUKAZI YAO


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi na wanafunzi wa Kijiji cha Mang’oto mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula katika Shule ya Sekondari Mang’oto linalojengwa kwa ufadhili wa TASAF, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani Njombe.

Baadhi ya wananchi na wanafunzi wa Kijiji cha Mang’oto wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati akizungumza nao mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula katika Shule ya Sekondari Mang’oto linalojengwa kwa ufadhili wa TASAF, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani Njombe.


Mbunge wa Makete, Mhe. Festo Sanga akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani Njombe.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi na wanafunzi wa Kijiji cha Mang’oto mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula katika Shule ya Sekondari Mang’oto linalojengwa kwa ufadhili wa TASAF, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya Makete.


Muonekano bwalo la chakula katika Shule ya Sekondari Mang’oto linalojengwa na Serikali kupitia TASAF katika Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani Njombe.

**********************

Na. Veronica Mwafisi-Makete

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka walengwa wa TASAF Wilayani Makete kuchangia nguvu kazi yao ya asilimia 10 ili kuwezesha ukamilishaji wa miradi ya TASAF ya ujenzi wa miundombinu kwa wakati katika Shule ya Sekondari Mang’oto ambayo inatekelezwa kwa ufadhili wa Umoja wa Nchi zinazosambaza Mafuta Duniani (OPEC).

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa walengwa wa TASAF, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Mang’oto iliyopo katika Kijiji cha Mang’oto, Halmashauri ya Wilaya ya Makete, mkoani Njombe.

“Wananchi wa Mang’oto nawaomba mjitoe kutekeleza miradi mbalimbali ya miundombinu inayowataka kuchangia nguvukazi yenu ya asilimia 10 ili mshiriki kukamilisha miradi hiyo kwa wakati,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada za kutafuta fedha kwa wadau wa maendeleo kuiwezesha TASAF kutekeleza miradi yake kwa lengo la kujenga miundombinu yenye tija kwa maendeleo ya taifa.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Makete, Mhe. Festo Sanga, amemhakikishia Mhe. Naibu Waziri Ndejembi kuwa, atawahamasisha wananchi wa jimbo lake wachangie nguvu kazi ili kuwezesha miradi yote ya TASAF inayotekelezwa katika jimbo lake ikamilike kwa wakati.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mang’oto, Bw. Prince Mwenda amesema, wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaboreshea mazingira ya kupata elimu kupitia ujenzi wa mabweni, madarasa, bwalo na nyumba za walimu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi anaendelea na ziara ya kikazi ya wiki moja mkoani Njombe kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF pamoja na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma mkoani huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments