VIJANA WATAKA KUUANA KISA BUKU


Shilingi elfu moja

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza, imefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa vijana wawili ambao walitaka kuuana kwa madai ya mmoja wao kushindwa kumlipa mwenzake shilingi elfu moja aliyokuwa amekopeshwa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Monica Ndyekobora amesema siku saba za maadhimisho ya wiki ya sheria moja kati ya migogoro waliyofanikiwa kusuluhisha katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Nyegezi, ni kwa vijana wawili ambao walitaka kuuana baada ya kukopeshana shilingi elfu moja

"Pale stendi mmoja alikuwa amebeba jiwe akitaka kumdhuru aliyekuwa anamdai na tulikuwa pale stendi tukawaita na kuwasikiliza wote, kwanza walikuwa hawataki kutulia na yule aliyekuwa anadaiwa alisema kwa muda huo hana hiyo shilingi elfu moja ndiyo akatuomba akafanye kazi akipata atakuja kulipa ndipo akaenda kufanya kazi alipoipata akaja kulipa tukaongea nao wakakubali kusameheana na kushikana mikono mgogoro ukawa umeisha kwa kuwasuluhisha," amesema Monica.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Dkt. Ntemi Kilekamajenga, amesema utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi umeingizwa kwenye sheria mwaka 1999 kupitia marekebisho ya sheria namba 11 ya mwaka 1999.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya sheria ya mwaka huu ni "Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau".

Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments