ASKOFU MABUSHI AONYA UCHUMBA KWA WANAFUNZI

Askofu wa Makanisa ya IEAGT Tanzania David Mabushi

Na Estomine Henry - Shinyanga

Askofu wa Makanisa ya IEAGT Tanzania David Mabushi ameonya wanafunzi kuwa na tabia ya mahusiano ya uchumba wakiwa bado wanasoma.


Akizungumza katika Ibada ya Jumapili Februari, 12 2023  Askofu aliwataka wazazi na walezi kuwakanya watoto kuhusu hali ya mahusiano ya uchumba wakiwa katika masomo.


Mabushi amesema,wanafunzi wengi wanashindwa kutimiza ndoto zao kwa kuanza mahusiano ya uchumba wakiwa kidato cha kwanza hadi cha tano huko shuleni kwa kudanganyana na kujikuta wanapata madhara kutoka kwa wenzao na watu nje ya shule.


Pia Mabushi alisema ,wanafunzi wengi wamebakwa,mimba za utotoni na kupata maradhi mbalimbali yaliyokwamisha kuendelea na masomo kutokana na mahusiano ya uchumba huko shuleni.


" Ndoto zenu hazitatimia nyie wanafunzi kwa tabia ya kuwa na mahusiano ya uchumba kabla ya umri sahihi, huu ni uongo wa shetani kuwadanganya ili kuharibu ndoto zenu",alisema Mabushi.


Aidha Mabushi, alikazia wazazi na walezi kuwa makini na tamthilia mbalimbali kwa kuwa ni mbegu ya kupanda fikra za mahusiano kwa watoto kabla ya umri wao.


"Najua hata wazazi na walezi ,mnapenda hizi tamthilia ila zina mtego mkubwa kwa watoto wenu,Ni vema kuchuja na kuweka msingi kipindi cha wao kutazama ,la sivyo tutaendelea kupata mabaya kwa hawa watoto maana si wote wana uwezo wa kupambanua uhalisia wa maisha ya kweli kwao", alisema Mabushi.


Kwa upande wazazi,Joshu Loibulu alisema, "Tunahitaji umakini kwa watoto na mengi machafu wanajufunza wao kwa wao ,sisi kama wazazi ni kuwa nao karibu kuwapa maadili mema."


Naye,Grace Kali alisema,Nyumba za ibada ni jukwaa jema kwa kutunza watoto kwa dunia ya sasa ili wawe na maadili mema na kuwa na hofu ya Mungu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments