PJFCS, POLISI, OFISI YA RC WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA, VYAKULA LISHE KUNUSURU AFYA ZA WATOTO WENYE UTAPIAMLO

Kikundi cha mazoezi (PJFCS), Polisi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika Hospitali ya Rufaa leo wakitoa masaada wa vifaa tiba, vyakula lishe kwa ajili ya kunusuru Afya za watoto wenye Utapiamlo, kupata miti na kuchangia damu.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KIKUNDI cha mazoezi cha Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, wametoa msaada wa vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kunusuru afya za watoto wenye Utapiamlo.

Msaada huo wa vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kunusuru afya za watoto wenye utapiamlo, vimetolewa leo Februari 20, 2023 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ikiwa ni malengo waliojiwekea ya kuanzisha Mbio za Shinyanga Madini Marathon ili kunusuru afya za watoto wenye Utapiamlo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shinyanga Madini Marathon Roland Mwalyambi, amesema Kauli mbiu ya mbio hizo za Shinyanga Madini Marathon ili kuwa ni 'Kimbia kwa afya saidia watoto wenye Utapiamlo', kwamba fedha ambazo watazipata zitakwenda kununua vifaa tiba na lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye utapiamlo.

“Mbio za Shinyanga Madini Marathon zilifanyika mwaka 2022 na fedha ambazo tulizipata tumenunua vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye Utapiamlo na leo tumevikabidhi hapa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga,"amesema Mwalyambi.

Naye Mlezi wa kikundi hicho cha mazoezi cha Polisi Jamii, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi, amesema uokoaji wa afya kwa watoto wenye utapiamlo ni faida kwa taifa, kwa sababu litapata vijana wenye akili na kuwa viongozi wazuri wa baadae.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dk. Kambi Buteta, ameshukuru kupewa vifaa tiba na vyakula lishe ambayo alisema vitakuwa msaada mkubwa kunusuru afya za watoto wenye Utapiamlo.

Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Dk. Yustina Tizeba, alisema tatizo la watoto wenye utapiamlo mkoani humo ni kubwa, lakini linaweza kuzuilika endapo wajawazito wakazingatia suala la lishe bora kipindi cha ujauzito wao.

Aidha, kikundi hicho cha mazoezi Polisi jamii wakiongozwa na mlezi wao Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi, wakiwa katika Hospitali hiyo pia walipanda Miti 100, pamoja na kuchangia damu salama.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kunusuru afya za watoto wenye Utapiamlo.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk. Kambi Buteta akizungumza kwenye makabidhiano ya vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya watoto wenye Utapiamlo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shinyanga Madini Marathon Roland Mwalyambi, akizungumzia utekelezaji wa ahadi yao ya kutoa msaada wa vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye Utapiamlo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (kushoto) ambaye ni Mlezi wa kikundi cha mazoezi cha PJFCS, akikabidhi vifaa tiba na vyakula lishe kwa ajili ya kuokoa afya za watoto wenye Utapiamlo, (kulia) ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Dk. Kambi Buteta.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (katikati) akiongoza zoezi la uchangiaji damu.
Uchangiaji damu ukiendelea.
Uchangiaji damu ukiendelea.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi (kulia) akizundua bustani ya matunda.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akiongoza zoezi la upandaji miti ya matunda katika eneo la Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.
Zoezi la upandaji miti ya matunda likiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha ya pamoja ikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post