MAFURIKO YAIKUMBA BRAZIL
Mamlaka katika jimbo la São Paulo nchini Brazil zinasema watu wasiopungua 36 wamepoteza maisha katika mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi, na kulazimisha baadhi ya miji kufuta sherehe za kila mwaka za Carnival.

Baadhi ya vitongoji vinaonekana vikiwa chini ya maji, huku barabara za magari zilizofurika na vifusi vikiwa vimeachwa baada ya nyumba kusombwa na maji.

Vikosi vya uokozi vimekuwa vikihangaika kuwafikia manusura na kufungua barabara. Mvua zenye kiwango cha milimita 600 zilinyesha katika baadhi ya maeneo siku ya Jumapili, mara mbili ya kiwango kilichotarajiwa kwa mwezi huu.

Serikali ya jimbo hilo imeripoti vifo visivyopungua 35 huko São Sebastião na Mamia wamekimbia makazi yao na wengine kuhamishwa.Wakati huo huo, maafisa wanasema watu wengine 228 wameachwa bila makao, huku wengine 338 wakihamishwa kutoka mikoa ya pwani kaskazini mwa São Paulo.Hali ya maafa ya siku 180 ilitangazwa katika miji sita katika jimbo hilo: São Sebastião, Caraguatatuba, Ilhabela, Ubatuba, Guarujá na Bertioga

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post