VIJIJI 11 WILAYANI KISHAPU HAVINA SHULE ZA MSINGI


Madiwani wilayani Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Madiwani wilayani Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Madiwani wilayani Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Na Sumai Salum, KISHAPU

Vijiji 11 Kati ya 125 wilayani Kishapu mkoani Shinyanga havina shule za msingi hali iliyoelezwa kuwa sababu ya kushuka kwa kuwango cha ufaulu shule za msingi kutoka asilimia 69%(2022) hadi 64% (2023).

Vijiji hivyo ni                  Butungwa,Igumangobo,Igaga"A",Bulekela,Mwampalo,Ng'wanholo,Lwagalalo,Ikonda "A",Ng'wagalankulu,Malwilo na Nhendegese.

Akiwasilisha taarifa ya elimu na kujibu hoja ya elimu kwenye kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili leo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Afisa elimu awali na Msingi Bw. Angasilini Obeid Kweka, amesema kuwa kwa kila vijiji ambavyo havina shule za msingi Serikali ya kijiji isimamie upatikanaji wa madarasa manne na matundu ya vyoo nane.

Kweka amesema kuwa Mpango Shirikishi jamii huu umekuja na Hoja ya uhitaji wa madarasa 800 kwa wilaya nzima kutokana na muitikio wa uandikishaji wanafunzi kuongezeka ambapo kwa darasa la awali wamesajili 94% na darasa la kwanza wamesajili asilimia 104% mpaka leo na bado wanaendelea na zoezi hilo hivyo uhitaji utaongezeka zaidi.

"Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na sababu sio walimu kama wengi wadhaniavyo bali watoto wetu wanatembea umbali mrefu jambo ambapo sio rahisi mtoto kuvumilia anatembea zaidi ya kilometa 10 kwa siku lazima achoke na wakati mwingine asiende shule kama akikosa masomo kwa siku kadhaa ni lazima atafeli tu na wakati wa mvua pia Barbara zetu sio rafiki hawafiki mashuleni", amesema Kweka.

Mbali na hayo wakijibu hoja hiyo Diwani wa Kata ya Songwa Mhe. Abdul Ngoromole amesema wako tayari kusimamia suala hilo kwani umuhimu wa elimu wananunua hivyo ofisi ya mkuu wa wilaya na mkurugenzi waharakishe utoaji maelekezo kwa viongozi wa vijiji na kata ili kufikia Desemba 2023 wawe wamekamilisha huku akishauri fedha za kunufaisha jamii zinazozunguka mgodi zielekezwe pia kwenye ujenzi wa madarasa.


Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Bunambiyu Mh. Mpemba Juma amesema pia kunahitajika kusimamia uundwaji wa bodi za shule kwani inasaidia kutatua changamoto zinazopelekea kushuka kwa ufaulu na usimamiaji wa Sheria ikilinganishwa na tukio la mwanafunzi kupata ujauzito na mwalimu mkuu Sekondari Bunambiyu kutoshirikisha mapema viongozi wa Kata hadi halmashauri wala jeshi la polisi.

"Mhe Mwenyekiti walimu hawa wanatakiwa wapunguziwe majukumu kwa mfano shule ya msingi Muguda ufaulu ni mbaya na hata shule ya msingi Beledi Mwalimu Mkuu wake ni Kaimu Mtendaji si rahisi akasimamia suala la ufaulu kabisa la sivyo ashushwe cheo", Mhe. Luhende Sana Diwani Kata ya Lagana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments