MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE WILAYANI KAHAMA IMEFANYA TUKIO LA UTAYARI JARIBIO LA AJALI YA NDEGE, WANANCHI WAPATA TAHARUKI

Zoezi la uokoaji abiria jaribio ajali ya ndege Kahama likiendelea.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

MAMLAKA ya viwanja vya ndege wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga imefanya zoezi la utayari juu ya jaribio la ajali ya ndege kuwaka moto, ili kujiweka tayari kutoa huduma ya uokoaji endapo likitokea tukio la ajali ya kweli ya ndege.

Tukio hilo la utayari limefanyika leo Februari 13, 2023 jirani na viwanja vya ndege wilayani Kahama kwa kuwashwa moto mfano wa ndege iliyoungua pamoja na baadhi ya watu kuigiza kuwa wamepata ajali kweli huku magari ya Zimamoto na ya wagonjwa wakipishana na kuleta taharuki kwa wananchi.

Akizungumzia tukio hilo Meneja wa uwanja wa ndege wilayani Kahama Hamza Kiyemo, amesema wamefanya tukio hilo la utayari wa jaribio la ndege kuwaka moto, ili kujiweka sawa endapo ajali ikitokea kweli wawe tayari kufanya uokozi na kuokoa maisha ya abiria.

“Kwa mujibu wa mwongozo wa uendeshaji wa viwanja vya ndege kitaifa, sheria ya anga mwaka 2006 inatutaka kufanya zoezi la uokoaji kila baada ya miaka miwili, lengo likiwa ni kupima uwezo wa taasisi, mashirika ya umma na binafsi, kutoa huduma za uokoaji pindi ndege inapopata ajali kwa kujiweka tayari,”amesema Kiyemo.

“Tukio hili la utayari linatufanya kuboresha huduma zetu pale inapoonekana kuwa dhaifu au hafifu, ili ajali ya ukweli ya ndege ikitokea tuwe tumejipanga sawa sawa kufanya huduma ya uokoaji, tunaomba radhi kwa wananchi wote ambao wameathirika kwa namna moja ama nyingine,”ameongeza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita, amesema tukio hilo la utayari wamejipima kuona jinsi gani walivyokamili katika kufanya uokozi hasa pale inapoweza kutokea ajali ya ndege.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto wilayani Kahama Inspekta Edward Selemani, amesema zoezi hilo la utayari limewafanya kubaini jinsi gani walivyojipanga kufanya uokozi hasa pale ajali ya ukweli ya ndege itakapotokea.

Nao baadhi ya wananchi wamesema tukio hilo la utayari limewashtua kwa sababu walishangaa kuona moto mkubwa umelipuka katika uwanja wa ndege huku magari ya kuzimia moto yakipishana pamoja na magari ya wagonjwa, na kuwafanya kuingiwa na hofu kuwa kuna ajali ya ndege imetokea.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumzia jaribio la utayari ajali ya ndege katika viwanja vya ndege wilayani Kahama.

Meneja wa uwanja wa ndege wilayani Kahama Hamza Kiyemo akizungumza tukio la utayari ajali ya ndege.

Mkuu wa kikosi cha Zimamoto na uokoaji wilayani Kahama Edward Salehe akizungumza tukio hilo la utayari ajali ya ndege.

Mwananchi Mariamu Punguja akizungumzia namna walivyopatwa na taharuki tukio la utayari ajali ya ndege.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Kahama wakizima mfano wa mabaki ya ndege katika tukio hilo la utayari ajali ya ndege.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Kahama wakizima mfano wa mabaki ya ndege katika tukio hilo la utayari ajali ya ndege

Zoezi la uokoaji abiria tukio la utayari ajali ya ndege likiendelea jirani na viwanja vya ndege wilayani Kahama.

Zoezi la uokoaji abiria tukio la utayari ajali ya ndege likiendelea jirani na viwanja vya ndege wilayani Kahama

Zoezi la uokoaji abiria tukio la utayari ajali ya ndege likiendelea jirani na viwanja vya ndege wilayani Kahama.

Wananchi wakiwa eneo la tukio la utayari ajali ya ndege wilayani Kahama.

Wananchi wakiwa eneo la tukio la utayari ajali ya ndege wilayani Kahama.

Zoezi la uokoaji abiria tukio la utayari ajali ya ndege likiendelea jirani na viwanja vya ndege wilayani Kahama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments