ASKARI POLISI ALIYEJERUHI VIBAYA MTOTO WAKE AENDELEA KUSOTA RUMANDE


Askari namba H.4178 Abati Benedicto wa kituo cha Polisi Bariadi anaetuhumiwa kumpiga hadi kumjeruhi vibaya mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 akitoka mahakamani baada ya kukosa dhamana.
Askari namba H.4178 Abati Benedicto wa kituo Cha Polisi Bariadi anaetuhumiwa kumpiga hadi kumjeruhi vibaya mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 akitoka mahakamani baada ya kukosa dhamana.
Na Mwandishi wetu, Bariadi.


Askari namba H.4178 Abati Benedicto wa kituo Cha Polisi Bariadi anaetuhumiwa kumpiga hadi kumjeruhi vibaya mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 jana amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Bariadi kujibu mashtaka yanayomkabili.


Ikumbukwe taarifa za Askari huyo kumfanyia vitendo vya kikatili mtoto wake, zilianza kuripotiwa katika vyombo vya habari baada ya tukio la Januri 15, 2023 la kumpiga mtoto wake maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumjeruhi vibaya.


Januari 23, 2023 Jeshi la Polisi kupitia taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Blasius Chatanda kwa waandishi wa Habari walikiri askari huyo kutenda tukio hilo na kueleza kuwa wanamshikilia kwa uchunguzi zaidi.


Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Mariam Nyangusi askari huyo alisomewa mashataka yanayomkabili na mwendesha mashtaka wa serikali Daniel Masambu ambayo ni kufanya ukatili dhidi ya mtoto.


Kesi hiyo namba 8/2023 ikisomwa kwa mara ya kwanza mwendesha mashtaka alieleza Mahakama kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo January 15, 2023 katika eneo la line polisi lililopo mtaa wa Malambo mjini Bariadi.


Masambu alieleza kuwa mtuhumiwa alimchapa mtoto wake kwa fimbo na kumjeruhi maeneo mbalimbali ya mwili wake kinyume na kifungu Cha 169 A kifungu kidogo Cha 1 na Cha 2 Cha Sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 marejeo ya mwaka 2022.


Hata hivyo mtuhumiwa alikana kosa hilo na kuelezwa na Hakimu kuwa dhamana yake iko wazi kwa masharti ya kuwa na fungu la dhamana ya sh. Mil 3 na wadhamini wawili wenye vitambulisho.


Mwendesha mashtaka alieleza mahakama kua tayari upelelezi umekamilika na kesi hiyo kupangwa kuanza kusikilizwa hoja za awali Machi 2 mwaka huu 2023.


Hata hivyo Mtuhumiwa hakutimiza vigezo vya kupata dhamana na amerudishwa rumande.

CHANZO - SIMIYU PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments