MBUNGE BUTONDO AMPA USHAURI OCD MPYA KISHAPU


Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo kulia,kushoto ni Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi wilayani Kishapu Ezibon Mathias.

Na Sumai Salum, KISHAPU

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo amemshauri Mkuu mpya wa Polisi wilaya hiyo (OCD) Ezibon Mathias kufanya kazi kwa ufanisi na weledi.

Ameyasema hayo leo 15.2.2023 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili ya halmashauri hiyo baada ya hivi Karibuni kupandishwa cheo kutoka Mkuu wa upelelezi wilaya hiyo hadi kuwa Mkuu wa Polisi wilaya.

"Wakati ukiwa Mkuu wa upelelezi ulikuwa unafanya sana kazi na pia wakati OCD aliyekuwepo akiondoka unapokaimu nafasi yake ulikuwa unatosha kile kiti, ndio maana umepandishwa cheo tunatambua pia utendaji kazi wako na tunatamani kutosikia tatizo la ubambikiaji kesi na mnatakiwa kuwa wepesi kufika eneo la tukio na uwaambie wasidizi wako kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia wananchi na sio kuwaumiza" amesema Butondo.

Aidha Butondo amemtaka Mkuu huyo wa Polisi  kuimarisha mahusiano katika kuboresha ulinzi wa wananchi na mali zao ndani ya jamii licha ya kukabiliwa na changamoto za uhaba wa magari.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu William Jijimya ameamuahidi Mkuu huyo wa Polisi kumpatia ushirikiano ili kuhakikisha amani inaendelea kutawala wilayani humo.

Kwa upande wake Mkuu huyo mpya wa Polisi wilayani Kishapu Ezibon Mathias ameomba ushirikiano kwa madiwani huku akiahidi kutokomeza masuala ya uhalifu wilayani humo, zikiwamo mimba na ndoa za utotoni. Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.
 
Mkuu mpya wa Polisi wilayani Kishapu Ezibon Mathias akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Meza kuu wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Baraza la Madiwani likiendelea.

Baraza la Madiwani likiendelea.
Baraza la Madiwani likiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments