SUMA JKT WAWASHA UMEME VIJIJI VITATU WILAYANI KISHAPU, DC MKUDE APONGEZA KASI YA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI

Uzinduzi wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMA JKT.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mkandarasi SUMA JKT ambaye anatekeleza mradi wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya tatu mzunguko wa Pili wilayani Kishapu na Shinyanga, ameanza kuwasha umeme katika Vijiji, Kaya na Taasisi za Serikali.

Zoezi hilo la uzinduzi wa kuwasha umeme limefanyika leo Februari 17, 2023 wilayani Kishapu, katika Kijiji cha Itilima Shule ya Msingi Isunda, huku vijiji vitatu vikiwashwa pia umeme ambavyo ni Itilima, Ikonokelo na Ipeja.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme wilayani Kishapu kwa vijiji hivyo vitatu, amesema amepongeza kasi ambayo wameanza nayo ya kusambaza umeme kwa wananchi na taasisi za Serikali, na kuwaomba waendelee na kasi hiyo hiyo ili kufikia Agosti mwaka huu vijiji vyote 51 wilayani humo viwe na huduma ya umeme.

“Shukrani SUMA JKT naomba muendelee na bidii ya kuunganisha umeme kwa wananchi na Taasisi za Serikali na ikifika Agosti vijiji vyote 51 wilayani Kishapu viwe na umeme na kuchochea maendeleo ya kiuchumi,”amesema Mkude.

“Tunampongeza Rais Samia kwa kutoa fedha na kutekelezwa miradi hii ya umeme vijijini ambacho kilikuwa kilio cha wananchi kwa muda mrefu lakini ndani ya utawala wake wa miaka miwili wananchi wa Kishapu wanapata umeme na leo tumewasha katika vijiji vitatu,”ameongeza Mkude.

Pia amewataka wananchi wa Kishapu ambao tayari wana huduma ya Nishati ya umeme walipie fedha TANESCO kwa ajili ya kuunganishwa umeme kwenye kaya zao na maeneo ya biashara.

Naye Meneja wa Shirika la umeme Tanzania mkoani Shinyanga (TANESCO) Mhandisi Leo Mwakatobe, amesema Shirika hilo litapeleka wataalam kwenye vijiji hivyo vilivyounganishiwa Nishati ya umeme ili kutoa elimu kwa wananchi na wajiunge kwa wingi kuunganishiwa huduma hiyo.

Meneja wa TANESCO wilayani Kishapu Mhandisi Elias Turnbull, amewaonya wananchi ambao tayari wana Nishati ya umeme kijijini kwao, wasije wakatumia vishoka kuunganisha umeme kwenye Kaya zao bali watumie wataalam kutoka TANESCO.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amesema amefurahishwa na kasi ya usambazaji umeme katika vijiji wilayani Kishapu, na kuwaomba wananchi wasihujumu mradi huo na kuiba miundombinu yake na kuiingiza hasara Serikali, huku akiwataka viongozi na Jeshi la Jadi Sungusungu kuhakikisha ulinzi unaimarika ili usifanyike wizi wowote wa vifaa.

Aidha, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya umeme kutoka SUMA JKT Major James Mhame, amesema kwa kasi waliyonayo ya kusambaza umeme vijijini wilayani Kishapu kwamba hadi kufikia Agosti mwaka huu vijiji vyote 51 vitakuwa na huduma ya Nishati ya umeme, pamoja na wilaya ya Shinyanga vijiji 50 ambapo huko wameshawasha umeme vijiji 10, Kishapu vijiji vitatu na wiki ijayo watawasha tena vijiji vingine.

“Kasi tuliyonayo ni nzuri tayari tumeshapokea nguzo za umeme 400 na zinakuja tena zingine 6,000 tunamuahidi Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan hatutamwangusha kwa kutuamini sisi SUMAJKT na kutupatia kazi hii ya kusambaza Nishati ya umeme vijijini na tutamaliza ndani ya muda,”amesema Meja Mhame.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Itilima Mkwaya Mwandu, amesema kupata huduma hiyo ya Nishati ya umeme Kijijini humo itachochea fursa za kiuchumi, na kuipongeza Serikali kwa kuanzisha mradi huo wa umeme wa REA vijijini.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu uliofanyika katika Kijiji cha Itilima katika Shule ya Msingi Isunda.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumzia namna SUMAJKT walivyo na kasi ya kusambaza Nishati ya umeme vijijini.

Diwani wa Itilima Lameck Nsubata akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu uliofanyika katika Kijiji cha Itilima katika Shule ya Msingi Isunda.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) mkoani Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akizungumza kwenye uzinduzi wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu uzinduzi uliofanyika katika Kijiji cha Itilima katika Shule ya Msingi Isunda.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilayani Kishapu Mhandisi Elias Turnbull akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa uwashaji umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu uliofanyika katika Kijiji cha Itilima katika Shule ya Msingi Isunda.

Mhandisi wa Mradi wa usambazaji Nishati vijijini (REA) Anthony Tarimo, akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa uwashaji umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu, uliofanyika katika Kijiji cha Itilima katika Shule ya Msingi Isunda.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya umeme kutoka SUMAJKT Major James Mhame, akielezea namna wanavyofanya kazi ili kuhakikisha wananchi katika vijiji 51 wilayani Kishapu wanapata huduma ya Nishati ya umeme wote ifikapo Agosti mwaka huu.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

SUMAJKT wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu.

Awali matengenezo yakiendelea ili kuwasha umeme katika kijiji cha Itilima wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

Awali matengenezo yakiendelea ili kuwasha umeme katika kijiji cha Itilima wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

Matengenezo yakiendelea ili kuwasha umeme katika kijiji cha Itilima wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

Matengenezo yakiendelea ili kuwasha umeme katika kijiji cha Itilima wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiwasha umeme katika shule ya Msingi Isunda-Itilima wilayani Kishapu ili kuzindua zoezi la uwashaji umeme katilka vijiji vitatu wilayani humo kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

Muonekano wa Taa ikiwa imewaka katika Ofisi ya Mwalimu Mkuu katika Shule ya Msingi Isunda-Itilima wilayani Kishapu.

Muonekano wa Taa zikiwa zimewaka katika Shule ya Msingi Isunda-Itilima wilayani Kishapu katika zoezi za uzinduzi wa uwashaji umeme katika vijiji vitatu wilayani Kishapu kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post