BARAZA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LIMEWAPATIA WAFANYABIASHARA BILIONI 3.5

 

Na Dotto Kwilasa, Malunde1 Blog-DODOMA.

BARAZA la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC)limewapatia zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 wafanyabiashara wenye viwanda vya kati na vidogo katika miradi 62 kwenye mikoa 12 nchini.

Hayo yameelezwa leo Februali 14,2023 Jijini hapa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Beng'i Issa wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya NEEC katika ukumbi wa habari Maelezo.

Amesema NEEC inasimamia majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi katika mikoa yote 26, na Halmashauri zote nchini ikiwa ni pamoja na kusimamia vikundi vidogo vya fedha pamoja na kuvilea pia kuvipa ushauri wa ni jinsi gani viweze kuendelea, jukumu hili limeanza tangu mwaka 2010 hadi sasa.

"Baraza huandaa Makongamano ya Kitaifa na Maonesho ya  Mifuko na programu za Uwezeshaji ili kuongeza na kukuza uwezo kwa walengwa ambayo  ni Kongamano la mwaka la Uwezeshaji, Kongamano la Ushiriki wa Wananchi katika Miradi ya Kimkakati, Maonesho ya mifuko na programu za Uwezeshaji,"amesema

Amesema,Baraza lina majukumu ya kuwezesha kubuni, kupanga, kusimamia, kufuatilia, kutathmini na kuratibu shughuli zote za uwezeshaji wa kiuchumi nchini na linafanya kazi kwa kufuata na kusimamia sera ya Taifa ya Uwezeshaji yenye nguzo mbalimbali ambazo.

Ametaja nguzo hizo kuwa ni pamoja na Ardhi ,Mitaji,Ushirika,Ubinafsishaji,Masoko na ujuzi na kwamba NEEC ndio chombo pekee kinachosimamia Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati (Local Content) hapa nchini.

Mkurugenzi huyo am├ęsema hadi sasa kuna kampuni zaidi ya 1,770 za Kitanzania zilizopata tenda katika miradi ya kimkakati na kufafanua kuwa watanzania zaidi ya 83,000 wamepata ajira katika miradi ya kimkakati hapa nchini.

"Baraza linasimamia na kuratibu mifuko na programu za uwezeshaji, hadi sasa nchini kuna mifuko zaidi ya 72, aina za mifuko inayosimamiwa ni pamoja na 
inayotoa mikopo moja kwa moja,  Mfano Women Development Fund, SELF Microfinance na Mifuko inayotoa dhamana, Mfano PASS Trust, Mfuko wa Nishati Jadidifu na inayotoa ruzuku, Mfano TASAF, Misitu Tanzania (TAFF),"amesema

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post