AZIKA MTOTO AKIWA HAI

 

Binti mmoja aliyejulikana kwa jina la Bright Okon, amemzika mtoto wake mchanga akiwa hai katika kaburi lisilo na kina alilolichimba kwenye bustani ndani ya boma dakika chache baada ya kujifungua akidai alikuwa hajui kama ni mjamzito.


Binti huyo, Bright (18), ambaye anaishi na wazazi wake katika nyumba ya kupanga, amesema hakujua kuwa alikuwa mjamzito hadi alipojifungua na alikiri kutenda tukio hilo jumatano ya Februari 15, 2023.


Baba yake, Okon Ekpenyong na majirani wanaofahamu kisa hicho, walisema, binti huyo ni muongo huku Mkunga, Elizabeth Okon anayeishi katika jamii hiyo, akithibitisha kwamba mtoto huyo alikuwa hai kabla ya kuzikwa.


Alipohiojiwa binti huyo alisema, “Mwili wangu ulikuwa ukiniuma ghafla nilianguka chini hapa (akionesha kwenye bustani eneo alilomzika mtoto), nikaona mtoto mchanga akitoka kwenye mwili wangu nikaanza kulia,” alisema Bright.

Alisema “nilipoteza fahamu nilipozinduka nilichimba shimo dogo la kumuweka mtoto nikasema mpaka mama arudi ndio nimuonyeshe,” na alipoulizwa kwa nini hakumpeleka mtoto ndani ya nyumba badala ya kumzika Bright alijibu hakujua la kufanya.


Tayari mamlaka za Serikali zinamshikilia Binti huyo kwa mahojiano, huku majirani wakikanusha madai kuwa mtoto alikuwa amefariki na ikibanika ukweli atafikishwa Mahakamani kujibu shutuma zinazomkabili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post