MFALME ZUMARIDI AFUTIWA KESI NA DPP


Mfalme Zumaridi

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP amesema hana nia ya kuendelea na kesi namba 11 ya mwaka 2022 iliyokuwa inamkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi ya usafirishaji haramu wa binadamu na kuomba shauri hilo kuondolewa mahakamani.

Wakili Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza Dorcas Akyoo, amesema DPP amefikia uamuzi huo kwa kifungu cha sheria namba 90 kifungu kidogo namba 11 sura namba 20 cha mwenendo wa mashahidi kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2022 ndipo Hakimu Mkazi Mwandamizi Bonaventure Lema, akamuachia huru Mfalme Zumaridi.

Mara baada ya umamuzi huo Wakili wa Serikali Dorcas Akyoo, akaiomba mahakama kupokea maombi ya serikali ya kumtaka Zumaridi awe chini ya uangalizi katika kipindi cha miaka mitatu bila kujihusisha na mambo yoyote ya uvunjifu wa amani ikiwemo na kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Mwanza mara moja kila mwezi.

Ikumbukwe Mfalme Zumaridi anatumikia kifungo cha mwaka mmoja baada ya kutiwa hatiani katika kesi namba 10 ya kuwazuia maafisa wa serikali kutekeleza majukumu yao, ambapo Mahakama ilimuamuru kutumikia kifungo cha mwezi mmoja gerezani baada ya kukaa mahabusu kwa muda wa miezi 11.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments