TAKUKURU SHINYANGA : HAKUNA DOSARI UJENZI WA MADARASA, BARABARA KUNA DOSARI

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga,Donisian Kessy

Na Halima Khoya,Shinyanga.

TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha robo pili ya mwaka wa fedha 2022/2022(Oktoba-Disemba,2022)  imeeleza jinsi ilivyojikita kwenye ufuatiliaji wa fedha za miradi kwa kutembelea ujenzi wa madarasa kwa shule zote za sekondari zilizopatiwa fedha na Serikali ili kuhakikisha fedha zilizoelekezwa katika miradi hiyo zinatumika kama ilivyokusudiwa,inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.


Akizungumza na vyombo vya habari leo Februari 16,2023 Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga,Donisian Kessy amesema jumla ya Shilingi Bil 6.6 (6,640,000,000/)= zimeletwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 332,ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa Kitaifa wa ujenzi wa madarasa 8,000 ya shule za sekondari ya mwaka 2022 ambapo ujenzi huo ulitakiwa kukamilika Desemba 30 2022.


Kessy amesema TAKUKURU ilifanya ufuatiliaji wa ujenzi wa madarasa 158 yenye thamani ya Shilingi Bil.3.3 (3,160,000,000/=) na haijabaini dosari mpaka sasa ambapo ufuatiliaji bado unaendelea.


Aidha TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga imefanikiwa kufuatilia Miradi ya maendeleo katika sekta za afya na barabara ambapo jumla ya Miradi ya maendeleo 10 imetekelezwa yenye thamani ya shilingi bil 3.6 (3,607,250/=) na dosari ndogo ndogo zilibainika.


“Mradi wa barabara ya mjini-Old Shinyanga inayotekelezwa chini ya usimamizi wa TANROADS,wenye thamani ya sh.700,010,000/= tulibaini kuwa kifusi cha subgrade layer G15 na sub base Course G25 (stabilized with cement) kimelipwa kwa urefu wa 1,080m badala ya 1,000m na kufanya mkandarasi kulipwa pesa ya ziada ya sh.12,240,000/= kwa kazi ambazo hazijafanyika,hali ya barabara ya mchepuo (diversion Road) siyo nzuri na inaathiri watumiaji”amesema Kessy.


“Ofisi ilifanya mawasiliano na meneja wa mradi TANROAD ambapo alitolea ufafanuzi kuwa wakati wa malipo walijulisha kazi ya barabara za mchepuo (access road/fider road) ambazo mkandarasi atazifanya mwishoni mwa mradi na kuahidi kuzingatia ushauri na kwa sasa barabara imerekebishwa na inapitika”ameongeza.


Kwa kipindi husika ofisi imefanya kazi za uchambuzi wa mfumo katika halmashauri (2) na Manispaa (1),(Ushetu,kahama na manispaa ya Shinyanga),ilifanyika warsha 3 na wadau husika kujadiliana mikakati ya namna ya rushwa iliyobainika na kuwekeana mikakati ya kutekeleza ili kumaliza mianya hiyo.


“Uwepo wa changamoto ya kamati ya kukusanya ushuru kwa kutumia risiti za mikono badala ya POS, changamoto ya mikataba iliyoingia manispaa juu ya uzoaji wa taka kutojulikana kwa kamati za soko,kuwepo kwa changamoto za masoko kutojua ni kiasi gani bajeti ya manispaa kinachorudi katika kuboresha miundombinu ya masoko na huduma nyinginezo katika utendaji wa masoko”amesema.


Takukuru imeweka hatua zitakazo chukuliwa kutatua adha hizo ambapo ukusanyaji wa fedha na michango yote itafanywe na kamati au watendaji wa Manispaa na ukaguzi maalumu wa mfumo wa upangishaji wa vibanda pamoja na kamati za elimu zipewe elimu juu ya usimamiaji wa uendeshaji wa masokona wahasibu wa mapato wapewe elimu.


“TAKUKURU inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali,kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa ubora,kama mtaona kuna vitendo vyovyote vinavyoonesha ubadhilifu vitoe taarifa”ameongeza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments