RUWASA, WAKANDARASI WATIA SAINI MIKATABA UJENZI MIRADI YA MAJI YA BIL 3.16 MASANGA – NDOLELEJI NA SESEKO - NGUNDANGALI

Utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga na Makampuni ya Wakandarasi Otonde Construction & General Supplies na Mponela Construction & Company Ltd wametia Saini Mikataba Miwili ya Ujenzi wa Miradi ya Maji Masanga – Ndoleleji na Seseko – Ngundangali yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.16 ikitarajiwa kunufaisha wananchi zaidi ya 38,751.

Hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali imefanyika leo Alhamisi Februari 16,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude na kushuhudiwa na wadau mbalimbali.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa ujenzi wa miradi hiyo, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude amewataka Wakandarasi hao kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo kwa uaminifu na uadilifu kwa viwango na ubora unaotakiwa kwa wakati.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude

“Miradi hii inatekelezwa kwa Fedha za serikali, naomba tushirikiane ili ilete tija kwa wananchi kwani lengo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama. Wakandarasi mkawe waaminifu na waadilifu, gharama zitumike hizo zilizopangwa ikibidi iwe chini. Pia nendeni mkakae vizuri na jamii, kalipeni vibarua,wafanyabiashara na watu mbalimbali mnaoenda kufanya nao kazi. Sitapenda kusikia malalamiko ya dhuluma”,amesema Mkude.

“Sina wasiwasi na RUWASA, wanafanya kazi vizuri. Waheshimiwa Madiwani naomba mkafuatilie miradi hii ikamilike kwa viwango,nendeni mkamalize migogoro midogo midogo itakayojitokeza badala ya kusubiri mpaka Mkuu wa wilaya aje. Uongozi wa wilaya upo imara, tutafuatilia. Sote tukashirikiane kwani hakuna kinachoshindikana tukishirikiana", amesema Mkude.

Akitoa taarifa kuhusu miradi hiyo ya maji, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima amesema jumla ya vijiji 9 na wananchi 38,751 wanaenda kunufaika na miradi hiyo mwili yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.16 inayotarajiwa kukamilika ifikapo Januari,2024.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima

Akielezea kuhusu Mradi wa Maji Seseko – Ngundangali, Mhandisi Kamazima amesema ujenzi huo utakaochukua muda wa miezi 12 kuanzia Februari 2023 hadi Januari 2024 unatekelezwa na Mkandarasi Kampuni ya M/S Otonde Construction & General Supplies Ltd kwa gharama ya shilingi 1,536,638,775/= na unatarajiwa kuhudumia wananchi wapatao 18,828 wa vijiji vitano vya Seseko, Mpumbula, Ngundangali, Kakola na Dugushilu.

Kuhusu Mradi wa Masanga – Ndoleleji, Mhandisi Kamazima unatekelezwa kuanzia Februari 2023 hadi Januari 2024 na Mkandarasi Kampuni ya M/S Mponela Construction & Company Ltd kwa gharama ya shilingi 1,626,581,254.20/= na utakapokamilika unatarajiwa kuhudumia wananchi wapatao 19,923 wa vijiji vinne vya Ndoleleji, Masanga, Mwampalo na Ng’wang’halanga.

Miradi hiyo itahusisha ujenzi wa matanki, vituo vya kuchotea maji,uchimbaji mitaro na ulazaji mabomba na ujenzi wa chemba mbalimbali,nyumba ya mitambo,kuunganisha umeme na kuweka pampu ya kusuma maji.

“Tunamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendo alionao kwa wananchi wa wilaya ya Kishapu hususani kwa kutupatia miradi ambayo itatuondolea kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama. Pia katika bajeti ijayo 2023/2024 jumla ya miradi 10 yenye zaidi ya shilingi Bilioni 7 inaenda kutekelezwa lengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini wawe wanapata huduma ya maji safi na salama kama ilivyoagizwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi”,amesema Mhandisi Kamazima.

Utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali.

Amesema licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na RUWASA kuhakikisha wanafikisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi, changamoto iliyopo sasa ni kuna maeneo mengine miradi hii inapoendelea kutekelezwa wameanza kupata vikwazo kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao hawataki mitaro ipite kwenye maeneo yao.

“Miradi yetu haina fedha za kulipa fidia. Nawaomba sana viongozi kila mmoja kwa nafasi yake tuweze kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa miradi hii. Waheshimiwa Madiwani miradi hii ya maji haina fidia ya maeneo tukawaelimishe pia wananchi wetu licha ya kwamba wataalamu wetu wanapita kuongea na wananchi katika mikutano ya hadhara”,ameeleza Mhandisi Kamazima.

Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela amesema RUWASA inaendelea kuboresha na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma ya maji safi, salama na usafi wa mazingira vijijini hivyo kuwaomba wadau wote kuendelea kutoa ushirikiano ikiwemo kulinda miundombinu ya maji.

Mhandisi Payovela amewataka wakandarasi kukamilisha ujenzi wa miradi ya maji kwa wakati wakizingatia ubora na viwango vinavyotakiwa kwa muijbu wa Mikataba waliyosaini.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.

“RUWASA tupo makini, tunataka miradi ijengwe ubora na viwango vinavyotakiwa. Tukamilishe ujenzi ndani ya muda uliopangwa kwa gharama zilizopangwa na kama kuna changamoto zinajitokeza tuambieni, msitufiche”,amesema Mhandisi Payovela.

Akizungumza kwa niaba ya Mkandarasi mwenzake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mponela Construction & Company Ltd, Dickson Mwipopo ameahidi kutekeleza mradi huo ndani ya muda uliopangwa huku akiomba ushirikiano kwa viongozi na wananchi.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo ameipongeza RUWASA kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maji wilayani Kishapu huku akiwahamasisha Wakandarasi kutiia sheria na kuzingatia mikataba, watekeleze kazi kwa wakati na wananchi wasishiriki kuhujumu miradi ya maji.

“Naomba tutunze miundombinu ya maji, tusihujumu kwani serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuleta fedha nyingi ili kuhakikisha tunamtua mama ndoo kichwani”,amesema Butondo.

Nao Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu, William Jijimya wamesema RUWASA inafanya kazi vizuri kufikisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi hivyo kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuruhusu mitaro ya maji ipitishwe kwenye maeneo yao na walinde miundombinu ya maji.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude  akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali iliyofanyika leo Alhamisi Februari 16,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude  akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali
Wadau wakiwa kwenye hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima akitoa taarifa ya ujenzi wa miradi ya maji wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mponela Construction & Company Ltd, Dickson Mwipopo (mwenye suti ya bluu kushoto) na  Mhasibu wa wa Kampuni ya Otonde Construction & General Supplies Ltd, Martine Nkomela  wakitia saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali

Zoezi la utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali likiendelea
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima (kulia) wakibadilishana nyaraka na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mponela Construction & Company Ltd, Dickson Mwipopo (mwenye suti ya bluu kushoto) na  Mhasibu wa wa Kampuni ya Otonde Construction & General Supplies Ltd, Martine Nkomela  baada ya kutia saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mponela Construction & Company Ltd, Dickson Mwipopo akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu, Mhe. Shija Ntelezu akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Mhe. William Jijimya akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali
Wadau wakiwa kwenye hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali
Wadau wakiwa kwenye hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali
Wadau wakiwa kwenye hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali
Wafanyakazi wa RUWASA wakiwa kwenye hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa maji Masanga – Ndoleleji na mradi wa maji Seseko – Ngundangali.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post