MGEJA AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI

Mkurugenzi wa Mgeja Shopping Centre Hamis Mgeja akiwa katika picha na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt. Jilly Elbariki Maleko muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya Uwekezaji ambapo Balozi huyo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwekeza nchini Burundi. Mhe. Mgeja yuko ziarani katika nchi za Burundi , Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji.

"Ninamshukuru na kumpongeza Mhe. Balozi kwa mapokezi mazuri na kutupatia ushauri Watanzania wanaotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi. Jumuiya ya Afrika Mashariki inatoa fursa za uwekezaji, ni muhimu tukaichangamkia fursa hii",amesema Mgeja.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post