RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU

 


Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri, ambapo amemhamisha Mohamed Mchengerwa aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumanne Februari 14, 2023 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Kabla ya mabadiliko hayo nafasi hiyo ya Waziri wa Maliasili na Utalii illikuwa ikishikiliwa na Dkt. Pindi Chana.Dkt. Pindi Chana amehamishiwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Pia Dkt. Samia amefanya mabadiliko madogo kwa Makatibu Wakuu wa wizara ambapo Dkt. Hassan Abbasi amehamishwa na kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii akitokea wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Profesa Eliamani Sedoyeka.

Said Othman Yakub ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Dkt. Abbasi.

Kabla ya uteuzi huo Yakub alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Viongozi hao wataapishwa hapo kesho saa 10 jioni Ikulu, Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments