MAAFISA TEHAMA, MAENDELEO YA JAMII WA HALMASHAURI WAPEWA MAFUNZO YA KANZIDATA YA TAIFA YA WANAWAKE NA UONGOZI TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu wameendesha Kikao na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania.

Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania ni mfumo rasmi wa kuhifadhi data mtandaoni ulioanzishwa ili kurekodi kuhifadhi na kusambaza wasifu wa wataalamu wanawake wa Kitanzania walioko ndani na nje ya nchi.

Akifungua kikao hicho, kilichofanyika leo Alhamisi Februari 23,2023 Mjini Morogoro, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi  ameishukuru TGNP kwa kushirikiana Wizara kutengeneza mfumo huo ulioundwa na vijana wa Kitanzania ambao utasaidia katika upatikanaji wa taarifa za wanawake ili kuhifadhi na kusambaza wasifu wa wataalamu wanawake wa Kitanzania.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi.
 
Amesema kuanzishwa kwa mfumo huo ni sehemu ya utekelezaji wa vipaumbele  vitano vya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ikiwemo kuwezesha ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi.

“Lengo la kikao kazi hiki kuwajengea uelewa maafisa maendeleo ya jamii na maafisa TEHAMA kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania ambapo kuufahamu vizuri mfumo huu itakuwa rahisi walengwa (wanawake) kujisajili kwenye mfumo. Naomba mkirudi kwenye maeneo yenu ya kazi mkawahamasishe wanawake wenye taaluma na ujuzi wajiunge”,amesema Mushi.

“Maafisa maendeleo ya jamii na TEHAMA tuna wajibu wa kuhamasisha jamii kuhusu mfumo huu, walengwa wajue umuhimu wa Kanzidata hii lakini pia wajisajili na mwisho wa siku ndiyo tutakuwa tunafanya mahubiri kwa vitendo kwamba tunawezesha wanawake kushiriki katika uongozi na ngazi za maamuzi”,ameongeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi amesema Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania imeanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili wa Wadau wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Sweden na Norway kupitia shirika la Norwegian Agency for Development Cooperation  (Norad).

“Uzinduzi Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania ulifanyika Machi 8,2022 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kitaifa yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Mfumo huu wa pekee wa kuweka wasifu wa wanawake wa Tanzania walioajiriwa katika sekta binafsi au serikali waliopo ndani nan je nchi umetengenezwa na vijana Wataalamu wa TEHAMA wa hapa Tanzania. Hii ni nyenzo kubwa  kwa ukombozi na kuleta usawa wa kijinsia”,amesema Liundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi 

“Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania itarahisisha taarifa za ajira katika sekta ya Umma na sekta binafsi. Mfumo huu utawezesha Serikali pamoja na waajiri wa ndani na nje ya nchi kama vile taasisi za kuajiri na kuteua, kutafuta na kupata wanawake wa Kitanzania wenye ujuzi, weledi na ubobezi katika taaluma mbalimbali kwa ajili ya mitandao ya kitaalamu na kuchaguliwa katika nafasi zilizo wazi katika nyanja na sekta zote. Naomba wanawake mtumie mfumo huu”,ameeleza Liundi.

Amewaomba Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA kutangaza mfumo huo wa pekee wa kuweka taarifa za wanawake wa Tanzania ili kuwafikia wanawake wengi zaidi huku akiahidi kuwa TGNP itazitambua Halmashauri zilizofanya vizuri kusajili wanawake wengi wakati wa Tamasha la Jinsia mwezi Septemba mwaka huu 2023.

“Nina imani kubwa kabisa kazi ambayo tumeijia hapa itasonga mbele katika kuendeleza masuala ya usawa wa kijinsia ambalo ni suala la maendeleo, wanawake ambao ni zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wa Tanzania   pamoja na makundi mengine huwezi kuwaacha nyuma katika mchakato wa maendeleo na ndiyo maana tuko hapa, twende wote kwa pamoja. Kikao hiki cha leo ni katika harakati za kuendeleza juhudi za kwamba wanawake wanashiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi na sote tunafahamu serikali ya awamu ya sita  ilisema bayana kwamba itaendeleza  juhudi za awamu zilizopita kuhakikisha kwamba wanawake na makundi mengine wanashiriki katika nafasi za maamuzi kwa vigezo vinavyotakiwa",amesema Liundi.

"Na kwa mantiki hiyo ndiyo maana tuna juhudi za kutengeneza Kanzidata hii kwa lengo la kuhifadhi kumbukumbu kuhusu wasifu wa wanawake wenye taaluma na ujuzi mbalimbali, nani amebobea kwenye nini, nani anachipukia kwenye nini na yuko wapi ili itakapofikia wanatafutwa kwa ajili ya kufanya kazi kwa manufaa ya nchi hii ya Tanzania hata nje ya Tanzania wajulikane kwa urahisi. Naomba wanawake wajiunge katika Mfumo huu kwa anuani ya https://twl.jamii.go.tz kwani pia mtandao huu utakuwa unatoa fursa mbalimbali zinazotokea katika sekta binafsi au serikalini”,ameongeza Liundi.

Nao Washiriki wa kikao hicho wameahidi kwenda kuhamasisha wanawake kujisajili katika mfumo huo kwa kukutana na makundi mbalimbali ya wanawake.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi akizungumza leo Februari 23,2023 Mjini Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania kilichoandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu. Picha na Kadama Malunde 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Afisa TEHAMA kutoka TGNP, Antweny Sawe akielezea jinsi ya kutumia mfumo wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania

Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, John Mapunda akiongoza majadiliano ya kuandaa mpango kazi wa kila wilaya kuhusu utekelezaji wa Kanzidata ya Taifa ya wanawake na uongozi Tanzania

Kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania kikiendelea
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.

Maafisa Maendeleo ya Jamii wakipiga picha ya kumbukumbu

Maafisa TEHAMA wakipiga picha ya kumbukumbu
Maafisa TEHAMA wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha na Kadama Malunde - Morogoro

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post