MBUNGE AFUKUZWA BUNGENI KISA SUTI YAKE INA ALAMA YA HEDHI


Seneta wa Kenya amefukuzwa bungeni baada ya kuhudhuria kikao akiwa amevalia suti nyeupe iliyokuwa na alama rangi nyekundu (kuashiria hedhi) katika kampeni inayoonekana kuwa ya harakati za kushinikiza upatikanaji wa taulo za hedhi.


Gloria Orwoba, wa muungano unaotawala, anatarajiwa kuwasilisha hoja kuhusu muswada wa kutoa taulo za bure siku ya Jumatano kama sehemu ya juhudi za kumaliza umaskini wa muda.


Maseneta walitatiza kikao cha Jumanne alasiri ili kumfahamisha spika kwamba Bi Owoba alikuwana "mavazi yasiyofaa".


Lakini seneta huyo alipinga akisema: "Nashangaa kwamba mtu anaweza kusimama hapa na kusema kwamba bunge limefedheheshwa kwa sababu mwanamke amepata hedhi."


Spika Amason Kingi aliamuru seneta huyo kwenda kubadilisha nguo zake kabla ya kuruhusiwa tena bungeni.

“Sio kosa kuwa na hedhi... Seneta Gloria nasikitika unapitia hali ya kimaumbile, suti yako imepata madoa ya ajabu, naomba uondoke ili ukabadilishe urudi na nguo ambazo hazina madoa," msemaji alisema.


Nje ya ukumbi, Seneta Owoba aliwaambia waandishi wa habari:


“Tunalenga kutokomeza janga linalotokana na unyanyapaa wa hedhi. Baadhi ya mambo ambayo ninayotetea ni kubuni sheria na kuhakikisha kwamba tunatoa bure taulo za hedhi kwa watoto wote wanaokwenda shule" ,amesema Gloria Orwoba



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post