YANGA SC YAENDELEA KUTOA DOZI ASFC, YAITUNGUA RHINO RANGERS 7-0


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TIMU ya Yanga SC imetinga hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuichapa mabao 7-0 klabu ya Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora.


Mechi hiyo ambayo ilipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam tumeshuhudia mchezaji wao mpya Yanga Sc Kennethy Musonda akipachika mabao mawili kwenye mchezo huo.


Yanga Sc ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Dickson Ambundo dakika za mwanzo kippindi cha kwanza huku bao la pili likifungwa na nyota wao Kennethy Musonda.


Mpaka dakika 25 ya mchezo kipindi cha kwanza Yanga Sc walikuwa mbele kwa mabao 5-0 na kwenda mapumziko wakiwa na mabao hayo ambayo mengine yalifungwa na Farid Mussa Yannick Bangala, David Bryson pamoja na Aziz Ki.


Yanga Sc iliwapumzisha baadhi ya wachezaji wao akiwemo Fiston Mayele, Dickson Job, Kisinda pamoja na baadhi ya wachezaji wengine ambao walikuwa na sababu mbalimbali kuukosa mchezo huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments