MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI RELI YA KISASA TABORA-ISAKA, AONYA POLISI KUJIHUSISHA NA WIZI WA VIFAA VYA UJENZIMkamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango (kulia) akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Reli ya kisasa kipande cha Nne Tabora-Isaka, (kushoto) ni Waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof Makame Mbalawa.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango, ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR), kipande cha Nne kutoka Tabora hadi Isaka.

Makamu wa Rais Dkt, Mpango ameweka jiwe la msingi leo Januari 18, 2023 katika ziara yake mkoani Shinyanga, pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ambapo kesho ataweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji ya Ziwa Victoria Tinde- Shelui.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Reli ya kisasa kipande hicho cha Nne, hafla ambayo imefanyika katika Kata ya Isaka Halmashauri ya Msalala, amewataka Wakandarasi kuukamilisha mradi huo kwa wakati na kiwango bora.

Amesema Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imedhamilia kuwekeza kwenye usafirishaji, ili kuboresha mazingira ya usafirishaji kwa miundombinu yake iwe rafiki kuwa imara, na kuingia kwenye ushindani wa kibiashara ikiwamo ujenzi wa Reli hiyo ya kisasa (SGR).

“Miradi hii ya kimkakati nataka isimamiwe vizuri isipotee hata senti moja, fedha hizi niza mkopo, na hakuna ubaya kukopa sababu tunazitumia kuleta maendeleo,”amesema Makamu wa Rais Dkt. Mpango.

Aidha, ameonya watu kujihusisha na wizi wa vifaa vya ujenzi kwenye ujenzi huo wa Reli ya kisasa, kwa kuiba mafuta, Nondo na Saraji, na kubainisha wizi huo umekuwa ukifanywa na wafanyakazi, madereva, waendesha mitambo, Askari Polisi, kwa kushirikiana pia na wananchi ambao wanaishi jirani mradi huo, na kuagiza mtandao wa wezi wote wasakwe na kuchukuliwa hatua.

Katika hatua nyingine amewaagiza Wakandarasi pamoja wasimamizi wa ujenzi wa mradi huo wa Reli ya kisasa, kuwa vipaumbele vya ajira na zabuni zote, wapewe wakazi wa maeneo husika ili wapate fursa na kuwainua kiuchumi.

Naye Waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbalawa, amesema ujenzi huo wa Reli ya kisasa (SGR), una manufaa makubwa katika nchi yetu, kwa kuboresha huduma za usafirishaji na kuokoa gharama, na kutolea mfano usafirishaji wa mizigo kwa njia ya Malori kutoka Dare es salaam hadi Congo ni siku 30, lakini kwa njia ya Reli ni saa 26 hadi 36.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa, amesema ujenzi huo wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Nne kutoka Tabora- Isaka ina urefu wa kilomita 165, na itakamilika Marchi 2026 kwa gharama ya Sh, Trilioni 2.6.

Mkamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango (kulia) akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Reli ya kisasa kipande cha Nne Tabora-Isaka, (kushoto) ni Waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof Makame Mbalawa.

Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu kwenye uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) Tabora -Isaka.

Kamati ya Amani ya Mkoa wa Shinyanga wakishuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR)Tabora-Isaka.

Wananchi na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye zoezi la uwekaji jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) Tabora-Isaka.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Philip Mpango akisalimia na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR),Tabora- Isaka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post