NGUMI YA 'SUGUNYO' YAMPA MANDONGA ZAWADI YA GARI


Bondia Mtanzania Karim Mandonga amekabidhiwa gari aliyoahidiwa endapo angeshinda pambano lake nchini Kenya, amepewa zawadi ya gari hilo aina ya Nadia na Mfanyabiashara Dick Sound bila masharti yoyote ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi aliyokuwa ameahidiwa endapo angeshinda pambano hilo.


Tukio hilo limefanyika leo hii katika Ofisi za DickSound Mall @dicksoundmall maeneo ya Magomeni Dar es salaam ambapo Dick amesema “Nimempa kama zawadi siyo kwa ajili ya Ubalozi, alikuja kwangu wakati anaenda kupambana nikamuahidi akishinda nitaweza kumpa gari, wakati akiwa Kenya nikaona video nikamtumia kumwambia umeniangusha ushapigwa, akasema hapana sio kweli Mimi ndio napanda kupambana, hivyo leo tumemkabidhi kumpongeza na kutimiza ahadi”.


Kwa upande wa Mandonga "Namshukuru sana DickSound Kwa hili leo ndoto yangu imetimia, Mandonga anaondoka na usafiri Mungu mkubwa".

Bondia huyo mwenye maneno na tambo za mbwembwe, alikuwa ameahidiwa gari iwapo angeshinda ndondi dhidi ya bondia Mkenya Daniel Wanyonyi.

Ushindi dhidi ya Wanyonyi ilikuwa mechi ya kwanza kwa bondia huyo kucheza nje ya Tanzania.

Licha ya Mandonga kupokea makonde mazito kutoka kwa wanyonyi katika raundi za kwanza, Mandonga alimwondoa Wanyonyi kwenye mechi baada ya kumzaba makonde mazito zaidi aliyoyapa jina la 'Ngumi za Sugunyo'.


Wanyonyi alishindwa kurejea uwanjani, uamuzi uliompa mandonga ushindi alioutabiri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post