MSICHANA WA MIAKA 14 AMUUA KWA KUMPIGA RISASI MVULANA WA MIAKA 11


Msichana mwenye umri wa miaka 14, alifikishwa kortini Jumatatu, Januari 16, kwa mashtaka ya mauaji ya mvulana mwenye umri wa miaka 11.

Marehemu alipigwa risasi wakati wasichana wawili walikuwa wakipigana, polisi wa Dallas, Marekani wanasema. 

Katika kisa hicho cha Jumapili, Januari 15, usiku, polisi waliitwa baada ya milio ya ufyatuaji risasi kusikika katika katika jumba la ghorofa kusini mwa Dallas.

Uchunguzi wa tukio hilo ulifanywa na kubainika kuwa wasichana wawili walikuwa wakipigana kwenye eneo la maegesho ya gari ya jumba hilo.

Kulingana na ripoti ya polisi wa Dallas, mshukiwa mmoja alichukua bastola na kumpiga risasi mwenzake aliyekuwa akipigana naye lakini risasi hiyo iliponyoka na kumpata mvulana aliyekuwa karibu.

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 11, alikimbizwa hospitalini ambapo alifariki kutokana na majeraha ya risasi.

Mshukiwa alikimbia kutoka eneo la tukio lakini baadaye alikamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Kwa sasa yuko chini ya ulinzi katika Kituo cha Haki cha Watoto cha Henry Wade, Marekani.

Silaha iliyotumika katika mauaji hayo ilipatikana wakati wa uchunguzi, ripoti ya polisi iliongeza.

Chanzo: Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post