MIKUTANO YA HADHARA VYAMA VYA SIASA YARUHUSIWA TANZANIA


-Rais Samia asema ni haki yao kikatba, akumbusha siasa za kistaarabu, kujenga nchi

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ametangaza rasmi kuruhusu kuanza kufanyika kwa mikutano ya vyama vya siasa nchini kuanzia leo.

Ametoa ruhusa hiyo leo Januari 3,2023 wakati wa kikao kati yake na vyama vya siasa nchini ambao kimefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba mikutano ya hadhara ni haki ya vyama vya siasa.

“Moja ya jambo ambalo limezungumzwa sana hata kwenye kikosi kazi ambacho nilikiunda kwa ajili ya kufuatilia hali ya kisiasa ni eneo la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.Hivyo uwepo wangu leo mbele yenu nimekuja kutoa ruhusa , kuja kutangaza lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoshwa.

“Vyama vya siasa ni haki kuendesha vyama vya siasa lakini tunawajibu kwa upande wa Serikali tumeshajipanga na wajibu wetu ni kulinda mikutano ya hadhara.Wajibu wa vyama vya siasa ni kufuata wajibu wa kufuata kanuni, niwaombe ndugu zangu tunatoa ruhusa twendeni tufanye siasa za kistaarabu, siasa za kujenga.

“CCM tuaamini kukoselewa na kukosoa, kosoeni, mimi naamini mkinikosoa najua changamoto iko hapa na changamoto niikifanyia kazi na kuitatua basi nitaendelea kuwepo.Ndio maana mimi siwaiti vyama vya upinzani bali ni vyama vinavyotuonesha kasoro,”amesema Rais Samia.

Hivyo amewaomba vyama vya siasa kwenda kuonesha siasa za kistaarabu, kufanya siasa siasa zenye kuheshimu mila na desturi.”Samia anaweza kuwa na uvumilivu , Samia anaweza kustahamili lakini chawa wa samia anaweza asistahimili.Vyama vya siasa nendeni mkaseme waliahidi hawajatekeleza.

“Kazi yetu itakuwa ni kutekeleza. Twendeni tukafanye siasa, kama tumekosea haki za binadamu tuambieni,lakini tukitukanana , tukaanza kurusha kashfa nchi haitakalika. Niwaombe ndugu zangu twendeni tufanye siasa, isemeni Serikali na ikosoeni .Ukiamua kupanda jukwaani jidhatiti na pale Serikali ambapo imefanya vizuri semeni.

“Najua mtakwenda kusema Serikali ina madeni lakini semeni madeni yamefanya nini, yanajenga SGR hadi Kigoma.Uongo haujengi, bali jengeni hoja, nimekaa na kuzungumza na vyombo vya ulinzi na usalama na vitawalinda lakini tukumbuke hakuna ambaye yuko juu ya Sheria.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post