RAPPA KANYE WEST AFUNGA NDOA NA MFANYAKAZI WAKERappa Kanye West 'Ye' kwa sasa ni mume mpya mjini! Ameripotiwa kuwa amefunga ndoa hivi karibuni, kwa mujibu wa TMZ.


TMZ imeripoti kwamba Kanye West amefunga ndoa na mfanyakazi kwenye kampuni yake ya Yeezy, bibie Bianca Censori ambaye ni mbunifu wa usanifu kwenye Kampuni hiyo.


Chanzo cha karibu na Kanye West kimeuthibitishia taarifa hiyo TMZ, hii ni baada ya kupata picha ya kidole cha Kanye West kikiwa na Pete ya ndoa.


Aidha, Kanye West na bibie Bianca Censori mapema wiki hii waliripotiwa kuonekana pamoja sehemu mbalimbali wakipata chakula.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post