WAREMBO WAWILI WAKAMATWA NA POLISI KWA KUPAMBA KEKI KWA PESA


Polisi wa Malawi wamewakamata wanawake wawili wenye umri wa kati ya miaka 20 baada ya kutumia noti za kwacha kama mapambo ya keki waliyokuwa wameoka na kuiweka kwenye mitandao ya kijamii.
Msemaji wa polisi alisema wawili hao walikuwa wamechapisha picha ya keki hiyo ikiwa imepambwa kwa noti 70 za 500 za kwacha - zenye thamani ya $35 (£28) kwenye mitandao ya kijamii walipokuwa wakitangaza biashara yao ya kutengeneza keki.

Washtakiwa hawajazungumzia kukamatwa kwao lakini polisi wanasema watashtakiwa kwa kosa la "kuharibu na kutumia fedha kinyume cha sheria".

Katika siku za nyuma, benki kuu ya Malawi imesema inaingia gharama kubwa kuchapisha noti mpya kuchukua nafasi ya zilizochakaa na kulaumu matumizi yasiyofaa ya noti kama moja ya sababu noti hizo kubadilishwa mara kwa mara.

Kosa la "matumizi mabaya na kinyume cha sheria ya sarafu" huadhibiwa kwa faini ya juu.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post