WABUNGE WA UPINZANI WATUPWA JELA KWA KUMPIGA MBUNGE MWENZAO


Wabunge wawili wa upinzani nchini Senegal, wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela na kulipa faini ya franc 100,000 za CFA (euro 150) kila mmoja sambamba na fidia ya faranga za CFA milioni tano (euro 7,625) kwa kumpiga mbunge mwenzao, Amy Ndiaye ndani ya Bunge.


Tukio hilo la ushambuliaji, lilifanyika Desemba mosi, 2022 baada ya Mbunge Massata Samb na Mamadou Niang kumshambulia Ndiaye kutokana na kauli alizotoa dhidi ya Kiongozi wa Muungano Mkuu wa Upinzani wa Party of Unity and Gathering, Moustapha Sy mwanariadha mwenye ushawishi mkubwa nchini Senegal.


Kufuatia shambulio hilo, Amy Ndiaye alilazwa Hospitali na yupo katika hatari ya kupoteza mtoto aliyembeba tumboni, huku wakili wake, Baboucar Cissé akisema wakati wa kesi licha ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, lakini bado yupo katika hali ngumu.


Wabunge hao wawili, waliokuwa kizuizini tangu Desemba 15, 2022 walihukumiwa rasmi Desemba 19 na Mahakama ya flagrante delicto ya jijini Dakar na picha zilizozagaa mtandaoni zilionesha zinaonesha Samb na Niang wakimpiga makofi na kumpiga teke la tumbo Bi Ndiaye aliyekuwa mjamzito wakati wa kikao cha Bunge

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post