WAZIRI GWAJIMA AKOSHWA NA MAENDELEO YA ISW KISANGARA


Kabla ya kuhudhurisha mahafali ya 5 ya @isw_official_tz #Kisangara Waziri Dkt. Gwajima alizindua rasmi madarasa mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 370 na ofisi mbili yaliyojengwa kwa fedha za ndani kwa kutumia wataalamu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai.

Aidha, ameweka pia jiwe la msingi katika ujenzi wa bweni la wanafunzi litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 104 na kuipongeza Taasisi @isw_official_tz kwa juhudi za ujenzi wa miundombinu katika kampasi hiyo zinazoendelea na utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Lulu Mahai ametoa wito kwa wadau wa malezi na makuzi kutumia Taasisi ya Ustawi wa Jamii kupata taaluma hiyo, huku akieleza kuwa Mipango ya muda mfupi ujao ni Kujenga Maktaba ya wanafunzi itakayo kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 na Kuanza kudahili wanafunzi wa Shahada ya Ustawi wa Jamii katika kampasi ya Kisangara.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Abdallah Mwaipaya ambaye aliambatana na Mh. Waziri Gwajima katika mahafali hayo amesema Taasisi @isw_official_tz #Kisangara imekuwa na manufaa kwa wilaya hiyo kutokana na kuendelea kupanuka kitaaluma hivyo ni msaada mkubwa kwenye jamii baada ya wahitimu hao kuwa tayari kuhudumia jamii, akiwafananisha na askari Miamvuli wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum watakao msaidia Mh. Waziri Gwajima kustawisha Tanzania.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post