WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA KAGERA WASHAURIWA KUTUMIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KWA KUPANDA MICHE BORA YA KAHAWA

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika KCU 1990 Limited Bw. Respicius John 
Zao la kahawa likiwa shambani

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Wakulima wa zao la Kahawa mkoani Kagera wameshauriwa kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda miche bora  ya kahawa ili waweze kunufaika na kilimo hicho.


Ushauri huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika Mkoa wa Kagera KCU 1990 Limited Bw.  Respicius John wakati akiongea na Malunde 1 Blog.

Amewataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanua mashamba ikiwa ni kung'oa ile miche iloyozeeka na kupanda miche mingine ili kuendana na ilani ya Chama Cha mapinduzi CCM mwaka 2020/25 inayosema kuwa ifikapo mwaka 2025 chama kikuu Cha ushirika KCU 1990 Limited kiwe kinazalisha takilibani tani laki tatu kwa mwaka ambapo kwasasa uzasharishaji wa chama hicho uko chini kwa kuzalisha kila mwaka tani 80 nchini kote.


Amesema kuwa Chama Kikuu Cha Ushirika KCU 1990 Limited kinajishugulisha na utafutaji wa masoko na kuongeza uzalishaji wa kilimo cha kahawa nchini Tanzania.

Bw. John amewashukuru wakulima mkoani Kagera kwa jitihada walizonazo katika kilimo cha kahawa na kuwa  katika msimu huu Chama hicho kimeweza kukusanya zaidi ya shiling Bilioni 110 ikiwa ni tani 50 za zao la kahawa.

Amewapongeza wakulima wa wilaya ya Kyerwa kwa kuzalisha Kahama ya zaidi ya shilingi Bilioni 59 kwa njia ya mnada na kufuatiwa wilaya ya Karagwe kwa kuzalisha zaidi ya shilingi Bilion 24  Wilaya ya Bukoba Vijijini zaidi ya shilingi Bilioni 10 wilaya ya Mleba zaidi ya shilingi Bilioni 4 wilaya ya Misenyi shiling Bilioni 10 wilaya ya Ngara wamezalisha zaidi ya shilingi Bilioni 5 na Bukoba mjini zaidi ya shilingi milioni 225 .


Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments