TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 61 YA UHURU HUKU MUASISI WAKE AKITIMIZA MIAKA 100 TANGU ALIPOZALIWA

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Na Dotto Kwilasa, Malunde 1 Blog.

LEO 9 Desemba 2022 ,2Tanzania inaadhimisha kumbukizi ya miaka 61 ya Uhuru wake huku muasisi wa uhuru huo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitimiza miaka 100 tangu alipozaliwa na Miaka 25 tangu alipofariki dunia.

Hata hivyo sherehe hizo zinafanyika bila kuwepo Kwa shamrashamra zozote kama ilivyo zoeleka na badala yake watanzania kuitumia siku hii kufanya makongamano ya  Midahalo na Makongamano mbalimbali  katika Wilaya zote hapa nchini kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea. 

Hatua hii ni baada ya Rais Samia kuelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya sherehe za uhuru ambazo ni milioni 960 kutumika kujenga mabweni na shule nane za msingi zenye wanafunzi maalumu.

Jambo hili pia lilifanywa na mtangulizi wake hayati Dkt.John Magufuli ambaye mwaka 2018 alielekeza fedha za uhuru kujenga hospitali mkoani Dodoma aliyopewa jina la Uhuru na kusaidia kutatua kero ya uhaba wa huduma za afya.

Kwa Mkoa wa Dodoma sherehe hizi zinaadhimishwa kwa kufanya usafi ambapo Jeshi la wananchi wa Tanzania limeonekana likifanya usafi katika maeneo ya hospitali ikiwa ni kutii agizo la Rais Samia.

Aidha Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT)umetumia siku hii ya Kumbukizi ya uhuru  Kwa kufanya kongamano la kumpongeza Rais Samia kukuza uzalendo 

Tanzania Bara ilipata Uhuru wake Desemba 09 ,1961 na tarehe 09 Desemba, 1962 ikawa rasmi Jamhuri hivyo kila mwaka Tanzania Bara husheherekea Maadhimisho ya uhuru ambapo kwa mwaka huu yameadhimishwa kwa kaulimbiu isemayo"Miaka 61 ya Uhuru:"amani na umoja ni nguzo ya maendeleo yetu".


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments