DUCE YAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA 

Wanafunzi wakiwa kwenye maandamano katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) leo Desemba 8,2022

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

JAMII yatakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inapinga masuala zima ya ukatili wa kijinsia kwani imekuwa ikikithiri kwa kiasi kikubwa kwenye jamii inayotuzunguka.

Akizungumza leo Desemba 8,2022 Jijini Dar es Salaam katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Naibu Rasi (Utawala, Fedha na Mipango) Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Dkt.Method Samwel wakati akimwakilisha Rasi wa Chuo hicho amesema katika maadhimisho hayo wamewashirikisha wanafunzi kikamilifu kutoa mafunzo miongoni mwao wenyewe juu ya ukatilli wa kijinsia na utoaji taarifa za ukatili.

Amesema wanaofanyiwa ukatili wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano na kushindwa kuchukuliwa hatua kwa wale ambao wamefanya ukatili wakihofia kudharauriwa na jamii inayomzunguka.

Amesema mwaka 1993 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio la kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake kupitia azimio namba 48/104, kuweka njia kuelekea kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana duniani kote.

"Mwaka huu, Duce kwa kushirikiana na UNESCO kupitia Mradi wake wa 03 Plus (Our Right, Our Lives, Our Future) tumeshirikiana katika kampeni hizi kikamilifu kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kuhusu ukatili wa kijinsia". Amesema

Pamoja na hayo amewapongeza UNESCO kupitia mradi wa 03 Plus kwa kuwashika mkono kwani nguvu yao imekuwa chachu katika utekelezaji wa kazi kama DUCE katika kupinga ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Afisa Msaidizi kutoka UNESCO (Idara ya Elimu ya Afya kwa Ustawi) Bi. Catherine Amri amesema ni wajibu wao kushirikiana na Serikali kuondoa changamoto ambazo zinakuwa vikwazo kwa wanafunzi kufikia elimu ya juu.

Amesema wamekuwa wakishirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii kuhamasisha vijana kuhakikisha wanatoa taarifa za ukatili na kutumia madawati ya jinsia yaliyoanzishwa katika vyuo vya elimu ya juu na kati.

Naibu Rasi (Utawala, Fedha na Mipango) Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Dkt.Method Samwel akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Desemba 8,2022 Jijini Dar es Salaam

Afisa Msaidizi kutoka UNESCO (Idara ya Elimu ya Afya kwa Ustawi) Bi. Catherine Amri akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Desemba 8,2022 Jijini Dar es Salaam Naibu Rasi (Utawala, Fedha na Mipango) Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Dkt.Method Samwel (katikati) akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Desemba 8,2022 Jijini Dar es Salaam Naibu Rasi (Utawala, Fedha na Mipango) Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Dkt.Method Samwel (katikati) akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Desemba 8,2022 Jijini Dar es Salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments