BARIDI YAUA WATU 19

Zaidi ya Wamarekani na Wakanada milioni moja wanasheherekea Sikukuu ya Krismasi bila umeme huku dhoruba kubwa ya msimu wa baridi ikiendelea kukumba Amerika Kaskazini.

Kimbunga 'bomb' kimeleta theluji, upepo mkali na baridi. Karibu watu milioni 250 wameathiriwa, na angalau vifo 19 vimehusishwa na dhoruba hiyo inayoenea zaidi ya maili 2,000 (3,200km) kutoka Quebec hadi Texas.

Maelfu ya safari za ndege zimehairishwakatika kipindi hiki cha sikukuu. Waapo waliokimbilia maeneo ya kusini kukimbia msimu wa baridi.

Jimbo la magharibi mwa Marekani la Montana ndilo lililoathiriwa zaidi na baridi, huku halijoto ikishuka hadi -50F (-45C). Hali mbaya imeripotiwa pia huko Minnesota, Iowa, Wisconsin na Michigan.

Katika jiji la Buffalo, jimbo la New York, Huduma ya Kitaifa ya Hali ya Hewa ya Marekani (NWS) iliripoti hali mbaya pia. Katika Pasifiki ya Kaskazini-Magharibi, wakazi wengine waliteleza kwenye barafu kwenye barabara zilizoganda huko Seattle na Portland.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post