BUNGE LAMFUKUZA KAZI RAIS KWA KUKOSA MAADILI


Jana Jumatano Desemba 7, 2022 inatajwa kuwa ni siku chungu kwa Rais wa Nchi ya Peru, Pedro Castillo ambaye amenyang’anywa tonge la ugali kinywani.

Bunge la Peru, kwa kauli moja limeamua kumuondoa madarakani Rais Pedro Castillo huku likipiga kura ya kumuweka Makamu wa Rais kwenye nafasi yake, muda mfupi baada ya kiongozi huyo kuidhinisha kuvunjwa kwa Bunge kabla ya kuchukuliwa hatua ya kumuondoa madarakani.


Ofisi ya mpatanishi mkuu wa kitaifa imelitaja jaribio la Rais Pedro Castillo la kuvunja Bunge kama mapinduzi, ingawa mtaalam mmoja wa kisiasa ametofautiana na wazo hilo.


Eduardo Gamarra ambaye ni mtaalam wa sayansi ya siasa na pia mhadhiri kwenye chuo kikuu cha kimataifa cha Florida amesema kwamba Bunge la Peru lina uwezo wa kumuondoa Rais madarakani, wakati pia Rais akiwa na uwezo wa kulivunja Bunge, kwa hiyo hatua ya Rais Castillo haikuwa mapinduzi.

Wabunge 101 dhidi ya 6 walipiga kura ya kuondolewa kwa Rais Castillo kutoka ofisini kwa madai ya utovu wa maadili, wakati 10 hawakushiriki kupiga kura.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments