SABABU KUU TANO KWANINI MBEGU ZA KIUMEKiwango cha mbegu za uzazi za kiume kinachotolewa wakati wa tendo la kujamiiana kimeshuka kwa asilimia 51 katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.


Ni moja ya matokeo makuu yaliyopatikana kufuatia uchunguzi uliofanywa na Chuo kikuu cha Hebrew cha Jerusalem, nchini in Israel, na katika Chuo cha tiba cha Mount Sinai, nchini Marekani.


Watafiti walifanya mahesabu na kubaini kuwa katika miaka ya 1970, wanaume walikuwa na wastani wa uzalishaji wa seli za uzazi milioni 101 kwa mililita ya ya majimaji ya mbegu za uzazi. Wastani huo umepungua hadi milioni 49 katika miaka ya hivi karibuni.


Zaidi ya idadi, ushahidi pia unafichua kupungua kwa ubora wa seli za uzazi za kiume: asilimia ya seli zenye uwezo wa kupenya na kuingia ndani ya yai la uzazi la kike zimepungua sana katika miongo ya hivi karibuni.


"Uwezo wa kutungusha mimba unapungua," anasema mtaalamu wa afya ya uzazi ya wanaume Moacir Rafael Radelli, na makamu rais wa Shirika la Brazil la madaktari wa uzazi wa kusaidiwa.


Hali hii inayoendelea kuwa mbaya inatoa dalili za hatari miongoni mwa wasomi katika sekta ya afya.


Kuanzia miaka ya 2000, kiwango hicho kilipanda hadi 2.64%: zaidi ya mara dufu.


Na ni tatizo katika dunia nzima : wanasayansi waligundua kupungua kwa idadi ya majimaji yanayohifadhi mbegu za uzazi za kiumbe Ulaya, Afrika, Amerika ya Kati na Amerika Kusini.


Je ni nini kinachosababisha hali hii? Wataalamu wanaeleza walau sababu tano. Habari njema ni kwamba kuna njia za kuzui tatizo hili .

1: Unene mwili wa kupindukia


Uzito wa mwili wa kupindukia huongeza athari kwa mbegu za kiume za uzazi.


Kuongezeka kwa ukubwa wa seli za mafuta, zinazomfanya mtu anenepe, husababisha majeraha mwilini -inflammatory, ambayo huathiri uzalishaji wa homoni za uzazi za kiume au testosterone, ambazo ni muhimu sana katika kutengenezwa kwa maji maji yanayotunza mbegu za kiume za uzazi.

Unene wa mwili wa kupindukia, vilevi na mlo usio kamili ni baadhi ya sababu zinazosababisha kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume za uzazi .


Daktari wa uzazi wa wanaume nchini Brazil Eduardo Miranda anasema uzito wa mwili wa kupindukia pia hutengeneza kile kinachoitwa oxidative stress , mchakato ambao huharibu seli mbali mbali za mwili.


"Kwa njia sawa na hiyo, mtu mwenye unene wa mwili wa kupindukia, huwa na mafuta zaidi katika maeneo ya viungo vyake vya uzazi, kitu ambacho huathiri vibaya utengenezwaji wa mbegu za uzazi za kiume ," anasema mtaalamu wa afya ya uzazi ya wanaume.


Manii, ambamo seli za uzazi hutengenezwa na kutunzwa, yanapaswa kuwa na kiwango cha joto cha cha nyuzi joto 1 hadi 2 wakati wote ili kufanya kazi vyema. Hii ndio maana mfuko huo wa mbegu za uzazi uko nje wa mwili.


Hii inaongeza mzigo wa mafuta kwenye viungo vya uzazi, ambavyo huacha kufanya kazi yake kama vinavyotarajiwa.


Shirika la Afya duniani linakadiria kuwa 39% ya wanaume wana uzito wa mwili wa kupindukia duniani, takwimu ambazo zinadhihirisha sababu ya kupungua kwa mbegu za uzazi za wanaume katika miongo mitano iliyopita.

2: Matumizi mabaya ya vilevi, na madawa ya kulevya


Pombe, sigara za kawaida, sigara za kielekroniki, bangi, Cocaine na dawa zenye anabolic steroid … Je unafahamu kuwa dawa hizi zote hutumiwa mara kwa mara? Zote huathiri viungo vya uzazi vya mwanaume.


"baadhi ya vilevi na madawa haya huharibu moja kwa moja seli za uzazi za kiume, ," anaeleza Dkt. Miranda.


Nyingine, hatahivyo, hua na madhara yasiyo ya moja kwa moja. Huathiri homoni za uzazi zinazochochea utendaji kazi wa manii(mfuko wa mbegu za uzazi za kiume)


Mfano unaotolewa zaidi miongoni mwa wataalamu ni kubadilishwa kwa testosterone kwa njia ya tembe, jeli, na sindano, ambazo hutumiwa na wanaume ili kuongeza ukubwa wa misuli.


Matumizi ya kupindukia ya sigara, pombe, na mihadarati huathiri afya ta mbegu za uzazi za kiume

3: Maambukizi ya magonjwa ya zinaa


Magonjwa kama vile Klamidia na chlamydia na kisonono, ambayo husababishwa na bakteria, yanaweza kusababisha majeraha katika njia ya mbegu za kiume iliyopo nyuma ya manii- epididymis.


Njia hii huunganisha sehemu ya juu ya manii na ni sehemu inayotunza mbegu za kiume za uzazi.


Madhara yoyote kwa sehemu hiyo, husababisha hatari kwa mbegu za kiume za uzazi.


Shirika la WHO linakadiria kuwa , katika mwaka 2020 pekee, kulikuwa na visa vipya milioni 129 vya maradhi ya chlamydia na visa milioni 82 vya kisonono miongoni mwa wanaume na wanawake. Kiwango hiki kimeendelea kuimarika na kuongezeka katika miongo ya hivi karibuni.


Radaelli anaongeza kuwa ugonjwa wa tatu ;kwenye orodha ya maradhi yanayosababisha kupungua kwa mbegu za kiume za uzazi ni : Ugonjwa wa virusi vya human papillomavirus, unaofahamika zaidi kama HPV.


"Pia unafahamika kwamba unaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu au hata Vinasaba DNA ya mbegu ya uzazi ," anasema.

4: Kompyuta kwenye mapaja


Unakumbuka kuwa manii yanapaswa kuwa katika hali ya hewa yenye kiwango cha katika ya 1-2°C baridi kuliko sehemu nyingine yoyote ya mwili ?


Tafiti zilizochapishwa katika miongo iliyopita zimefichua kuwa kubeba kipakatarishi chako au laptop kwenye paja kunasababisha hatari ya ziada katika uzalishwaji wa mbegu za kiume za uzazi.


Hii ni kwasababu betri ya kifaa hicho hupata joto na inaweza "kupika" mbegu za kiume.


Kuweka kipakatarishi kwenye mapaja kwa saa nyingi kunaweza ‘’kupika’’ mbegu zako za kiume za uzazi


Kuweka kipakatarishi kwenye mapaja kwa saa nyingi kunaweza ‘’kupika’’ mbegu zako za kiume za uzazi


Miranda anasema kwamba tabia nyingine zinazohusiana na viwangi vya juu vya joto pia husababisha hatari kwa viungo vya uzazi.


Kwa mfano, kuoga kwa muda mrefu maji moto au kuingia katika sauna kwa saa nyingi.


Pia katika sekta ya teknolojia, daktari alielezea uwezekano wa mawimbi ya kielekroniki , mawimbi ya simu na hata intaneti ya Wifi.

5: Kemikali za sumu za Endocrine disruptors


Wataalamu wanatahatharisha pia kuhusu msururu wa kemikali za sumu zinazofahamika kwa ujumla kama endocrine disruptors.


Kemikali hizi ni pamoja na zile zinazochafua hali ya hewa, pamoja plasiki na kemikali za kuua wadudu.


Kwa ujumla, sumu hizi zina muundo sawa na ule wa homoni katika miili yetu.


Zaidi ya mazingira na sababu nyingine zinazosababisha kupungua kwa kiwango cha mbegu za kiume za uzazi, kuna mambo mengine yanayochangia hali hii.


La kwanza ni urithi. Inakadiriwa kuwa 10 katika 30% ya visa vya ugumu katika kupata mtoto husababishwa na matatizo katika vinasaba DNA vya kiume .

Kiwango fulani cha mbegu za kiume zenye kasoro pia kimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.


Sababu ya pili inahusiana na umri na ukweli kwamba wanaume hutaka kuwa wazazi baada ya umri kuwa mkubwa, baadaye maishani mwao.


"Tunafahamu kuwa uwezo wa kutungisha mimba hupungua kadri miaka inavyokwenda. Ingawa kupungua kwa mbegu za kiume za uzazi miongoni mwa wanaume haulinganishwi na wanawake, huwa kuna upungufu katika homoni ambazo ni muhimu kwa utengenezaji wa mbegu za kiume ," anasema mtaalamu.

Nini la kufanya?


Kwa wale ambao wanataka kupata watoto, hatua ya kwanza ya kuongeza nafasi za kupata mtoto ni kufanya mabadiliko katika mtindo wa maisha unayoishi na hivyo kupunguza mchakato unaodhuru manii (mfuko wa dmbegu za kiume za uzazi)


Hii ni pamoja , na kwa mfano kuimarisha au kupunguza uzito wa mwili kwa kula mlo kamili na kufany amazoezi ya mara kwa mara ya mwili. Kuepuka pombe, sigara na madawa mengine pia ni mambo ya msingi yanayoshauriwa uyafanye.


Watu wanaopata chanjo dhidi ya HPV katika miaka yao ya kwanza ya kubalehe pia hujikinga zaidi dhidi ya virusi hivyo na madhara vinavyosababisha kwa mwili.

Inashauriwa kupata ushauri iwapo tatizo la kukosa mtoto linaendelea


"Iwapo una umri wa chini ya miaka 35, wenzi wanapaswa kuwa na mtoto kwa hadi mwaka mmoja, kwa kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, walau mara tatu kwa wiki , huku wakifuatilia kipindi cha utungwaji wa mimba," anasema Miranda.


Hatahivyo, iwapo wenzi wana umri wa zaidi ya miaka 35, kushindwa kupata ujauzito kwa zaidi ya miezi sita ni tahadhari kwao, na wanapaswa kupata ushauri wa kimatibabu.


Kama tatizo ni la upande wa mwanaume, wataalamu kwa kawaida humshauri mwanaume kupata dawa mbadala zenye uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini, ambazo pia husaidia kuyalinda manii yake (mfuko wa mbegu za kiume za uzazi).

CHANZO- BBC SWAHILI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post