MOROCCO YAIANDIKIA HISTORIA AFRIKA... YAFUZU NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA


Na Mwandishi Wetu


Wawakilishi wa bara la Afrika katika Michuano ya Kombe la Dunia, timu ya taifa ya Morocco imefuzu hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Ureno.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Al Thumama nchini Qatar, bao la Morocco limefungwa na En-Nesyri kwenye dakika ya 42’ katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Morocco wakiwa bora na nidhamu ya ulinzi ya hali ya juu katika Michuano hiyo walifanikiwa kuwazuia Ureno waliokuwa wakilisakama lango lao kwa muda mrefu hususani katika dakika 45’ za kipindi cha pili wakiwa na Nyota wao maarufu, Cristiano Ronaldo, Joao Felix, Pepe na wengine wengi.

Kwa matokeo hayo, Morocco imeandika historia katika Michuano hiyo kwa kuwa timu ya kwanza barani Afrika kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post