BWANA HARUSI AJIUA SHAMRA SHAMRA ZA SHEREHE ZIKIENDELEA UKUMBINI JIJINI MWANZA


Sherehe ya harusi kati ya Swadiku Abas (50) na mke wake, Elieth Rwegashora (40) ambao ni wakazi wa Mtaa wa Zenze eneo lililopo Kiseke wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, iligeuka msiba baada ya bwana harusi kujinyonga muda mfupi kabla ya sherehe kuanza.


Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani hapa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumamosi Desemba 24, 2022, tukio hilo lilitokea Desemba 17, 2022, muda mfupi baada ya wawili hao kufunga ndoa katika msikiti wa Swadikul Amiin.


Taarifa hiyo iliyosainiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa imeeleza kwamba sherehe ya ndoa hiyo iliyoingia dosari ilipangwa kufanyika katika ukumbi wa Mtena B lililopo eneo la Buzuruga jijini Mwanza na wakati taarifa za kifo hicho zinapatikana, ndugu, jamaa, marafiki na waalikwa tayari walikuwa ukumbini.

Chanzo - Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post