MWANDISHI WA HABARI WA TBC JOACHIM KAPEMBE AFARIKI KWA BAISKELI MLIMA KILIMANJARO

Mwandishi wa habari na mpiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mkoani Manyara Joachim Kapembe amefariki dunia alipokuwa akishuka kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa ambaye ni mmoja waliopanda na Joachim Kapembe (Mwandishi wa Habari wa TBC) kwenye  mlima Kilimanjaro, amesema Kapembe amefariki dunia kwa ajali ya baiskeli akitoka kambi ya Kibo kuelekea kambi ya Horombo baada ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa mafanikio.

Kapembe pamoja na watendaji wengine wa wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari walipanda kwenye mlima Kilimanjaro tarehe 9 mwezi huu kwa ajili uzinduzi wa intaneti ya mwendokasi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Alizaliwa tarehe 26 Februari mwaka 1977 wilayani Muheza mkoani Tanga.

Aliajiriwa na TBC Oktoba Mosi mwaka 2011 kwa cheo cha mpiga picha daraja la II.

Hadi anafariki dunia tarehe 13 mwezi huu alikuwa na cheo cha mpiga picha mkuu daraja la I.

Joachim Kapembe ameacha mke na watoto wawili.

Chanzo - TBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post