DIT NA TEMDO WASAINI MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA ILI KUZALISHA BUNIFU ZILIZO BUNIWA NA TAASISI HIZO KIBIASHARA


Wakuu wa Taasisi ya usanifu na ubunifu mitambo ( TEMDO) na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DTI) wakibadilishana mikataba mara baada ya kutia saini ya makubaliano ya kufanya kazi kwa kushirikiana kwa lengo la kuendeleza na kuzalisha bunifu zilizobuniwa na Taasisi hizi kibiashara.

Na Woinde Shizza , ARUSHA


Taasisi ya teknolojia Dar es salaam (DIT) kwa kushirikiana na Taasisi ya usanifu na ubunifu mitambo (TEMDO) wamesaini makubaliano ya kufanya kazi kwa kushirikiana kwalengo la kuendeleza na kuzalisha bunifu zilizo buniwa na Taasisi hizi kibiashara.



Taasisi ya DIT imekuwa ikifanya bunifu nyingi lakini zimekuwa zikishidwa kufanyiwa kazi kutoka kwenye natharia kwenda kwenye uhalisia hivyo mashirikiano hayo yatasaidia bunifu nyingi zilizowekwa muda mrefu kufanyiwa kazi kwani temdo wanawataalam wengi pamoja na mashine nyingi za kutengeneza bunifu hizo kwenda kwenye uhalisia.


Akiongea wakati wa utiaji Saini katika makubaliano hayo mkuu wa taasisi ya DIT Profesa Preksedis Marco Ndomba alisema kuwa makubaliano haya ni muarobaini wa Vifaa Tiba vya hospitali kwani wanazo bunifu zilizopo tayari ambazo zitazalishwa kibiashara kwenye karakana ya vifaa tiba ya Taasisi ya TEMDO kwani kwa sasa inazalisha vifaa Tiba vyenye Ubora na Viwango uliodhibitishwa na MSD na TMDA.


"Tukiambatana nao maana yake ni kama wana tushika mkono kwenye mandate kama watazikubali tafiti zetu tutakazo waletea hama tukikubaliana kuboresha baadhi ya bunifu basi maana yake zinaweza kufika huko zinapohitajika , tuna tafiti nyingi sana tumefanya kama nilivyosema na zipo nyingi sana",alisema.


Aidha alisema kuwa pia wana bunifu nyingi sana za vifaa tiba walizozifanya hivi karibuni na kwa kuwa temdo wamepata jukumu la kutengeneza vifaa tiba na wao bunifu walizonazo za vifaa tiba ni zile bunifu ambazo hatua zilizo fika tumeridhika nazo kwamba zinaweza kuendelezwa kirahisi na Temdo na kuweza kuwafikia wananchi kwa urahisi.


Alisema kuwa katika taasisi yao wame anzisha chumba maalumu cha kuhifadhi hizo bunifu lakini mara nyingi zinaishia pale kwasababu kwanza hawana vifaa machine zile za kuendeleza zile bunifu kama walizokuwanazo Temdo pia hawana baadhi ya wataalamu ambao wanaoweza kuzipeleka hizo bunifu kwenye hatua ya kuendelezwa na kuweza kutumika kwenda kutengeneza bidhaa ambazo zinaweza kutumika kwenye viwanda vidogo vya kati na vikubwa.

Alibainisha kwamba vile vifaa tiba au bunifu walizo nazo ni zile za kuwafikia wananchi wa hali ya chini pia tunajaribu kuhakikisha kwamba teknolojia zote ambazo zinaendelezwa pale ni zile ambazo zinaweza kupatikana na wananchi hasa ni kwenye zile hospitali za mbali kama vijijini.



" Mimi na matumaini yangu kwamba sasa nina fikiri uhusiano huu ni muharubahini wa kuacha kununua vifaa tiba nje ya nchi ambapo hile tabia ya kuendelea kununua vifaa kutoka nchi za nje sasa nafikiri ndo mwanzo wa kuachana na bidhaa kutoka nje hapo awali tulikuwa tunanunua kwa sababu tulikuwa hatushirikiani kwa hiyo tulikuwa tunashindwa kupambana na watu wa nje lakini kwa ushirikiano huu naamini kabisa tunamaliza tatizo la vifaa tiba", alisisitiza.



Kwa upande wake mkurugenzi Mkuu wa TEMDO Mhandisi , Profesa Fredrick Kahimba alieza kuwa makubaliano hayo yatasaidia watafiti wa TEMDO na DIT kufanya kazi za kitafiti Kwa pamoja ikiwa nipamoja na kubalishana Watalamu kwa lengo la kijifunza na kuwaongezea umahiri.



"Kwa hiyo hizi taasisi zimekutana kushirikiana kupata uzoefu walicho kuwa nacho wao sisi hatuna na tulichonacho sisi wao hawana sio hawana kabisa ni kwa wingi au kwa ubora kama nilivyosema awali kwamba taasisi ya teknolojia ya sanifu na ubunifu mitambo inafahamika kwa kuja na bunifu mbalimbali na nyingi kwa ajili ya kumsaidia mwananchi",alisema Kahimba.



Naye mwenyekiti wa bodi ya TEMDO Dkt. Richard Masika aliwapongeza kwakuingia katika mashiriano hayo na kuwataka kufanya kazi waliokusudia Ili kuweza kuwasaidia wananchi na kuwasihi kutoingiza siasa yoyote katika makubaliano hayo ambapo pia aliwataka wawe vichocheo kwa ajili ya maendeleo ya viwanda hapa nchini .



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments