ASKARI POLISI WAFARIKI WAKIELEKEA MSIBANIWanandoa waliofariki dunia

Wanandoa wawili ambao wamefunga ndoa Desemba 17, 2022, wamefariki dunia juzi Desemba 20,2022 kwa ajali ya gari baada ya kulivaa kwa mbele basi la kampuni ya Luwinzo lililokuwa likitokea mkoani Njombe kuelekea Dar es Salaam, katika eneo la Tanangozi mkoani Iringa.

Wanandoa hao wote walikuwa ni watumishi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, na walifariki dunia wakiwa njiani kuelekea jijini Mbeya kwenye msiba na juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa zinaendelea.

Imeelezwa pia kuwa kwenye gari walilokuwa nalo alikuwepo mama mzazi wa mmoja wao, na kwamba alipata majeraha makubwa katika miguu yake miwili na anapatiwa matibabu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema ilisababisha vifo vya watu watatu na majeruhi wawili ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali mkoani humo.

CHANZO - EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post