GCI YAWANOA MABALOZI WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA SHINYANGA.... "ACHA UKATILI"

Mjumbe wa Bodi katika shirika la GCI, Fabian Stephano Kalabwe akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Shirika la Green Community Initiatives (GCI) limefunga mafunzo ya siku tano (5) kwa mabalozi ngazi ya jamii wa kata ya Itwangi, Lyamidati na Nsalala huku washiriki hao wakiagizwa kuutekeleza ipasavyo mpango kazi unaolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Shirika hilo la GCI linatekeleza mradi wa “ACHA UKATILI” katika kata ya Itwangi, Lyamidati na Nsalala Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kupitia ufadhili wa shirika la Women Fund Tanzania Trust kwa lengo la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mafunzo hayo yalianza Novemba 28 na yamehitimishwa leo Desemba 2,2022 ambapo Mjumbe wa Bodi katika shirika la GCI, Fabian Stephano Kalabwe amewasisitiza mabalozi hao kwenda kutoa elimu hiyo kwenye jamii ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

“Muende mkaifundishe jamii kwa juhudi kwa yale mliyofundishwa kupitia vijiwe vya Kahawa, kupitia vijiwe vya bodaboda, wazazi wa kike na wa kiume pamoja na watoto, vikundi vya Hisa, Vikoba lakini pia kwenye mikutano ya hadhara na ikiwezekana kupitia madhehebu ya dini mkipana nafasi hiyo msiogope kutoa elimu”, amesema Kalabwe

“Katumieni mbinu za ufundishaji, katumieni Lugha ya mawasiliano ili muweze kuwasiliana vyema na jamii nendeni mkashirikiane, kazingatieni mpango wa kazi ambao mmefundishwa na mkautekeleze ipasanyo kwa wakati, kuweni na nidhamu, kuweni na heshima, mkawe wanyenyekevu na mkawe waaminifu mbele ya jamii ili kazi yenu iweze kuwa rahisi, nendeni mkajiamini na mkafanye kazi kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali ngazo zote natumaini mkifanya hivyo mtafanikiwa”, amesema Mjumbe wa Bodi Kalabwe

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Shinyanga  Aisha Omary amewataka mabalozi hao kwenda kuibua vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto huku akiwasisitiza kuzingatia maelekezo ya serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aisha Omary ambaye pia ni Mratibu wa mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) amewasisitiza kwenda kutoa elimu ya ukatili kwenye jamii ili kuimarisha uchumi wa kaya.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Green Community Initiatives (GCI) Mkoa wa Shinyanga Bwana Ngolelwa Enos Masanja ameeleza kuwa shirika hilo limetoa mafunzo kwa mabalozi 8 wa kata ya Itwangi, Lyamidati na Nsalala ambapo ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa mabalozi hao pale watakapofika kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yao.

“Tunachokiomba katika serikali za mitaa kule ambako watapita muweze kuwa ushirikiano ili kusudi waweze kuifikia jamii kama vile ambavyo tumelenga katika kuhakikisha jamii inakuwa na usawa ili kutokomeza kabisa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto”, amesema.

Mabalozi waliohudhuria mafunzo hayo wamewashukuru wawezeshaji huku wakiahidi kuzingatia maelekezo yote waliyopewa na kwamba wataifikia jamii kwa lengo la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Mjumbe wa Bodi katika shirika la GCI, Fabian Stephano Kalabwe akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mjumbe wa Bodi katika shirika la GCI, Fabian Stephano Kalabwe akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Shinyanga vijijini ambaye pia ni mratibu wa mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA)Aisha Omary akizungumza kwenye mafunzo hayo

Meneja wa Shirika la Green Community Initiatives (GCI) Mkoa wa Shinyanga Bwana Ngolelwa Enos Masanja akizungumza kwenye mafunzo hayo
Meneja wa Shirika la Green Community Initiatives (GCI) Mkoa wa Shinyanga Bwana Ngolelwa Enos Masanja akitoa maelekezo kwa mabalozi ngazi ya jamii.Mabalozi ngazi ya jamii wakiendelea kupewa maelekezo juu ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments