Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akizungumza katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani, kufungua mashindanoya insha na kufungua warsha ya wadau katika uandaaji wa viwango iliyofanyika leo Novemba 18,2022 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akizungumza katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani, kufungua mashindanoya insha na kufungua warsha ya wadau katika uandaaji wa viwango iliyofanyika leo Novemba 18,2022 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani, kufungua mashindanoya insha na kufungua warsha ya wadau katika uandaaji wa viwango iliyofanyika leo Novemba 18,2022 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Uandaaji wa Viwango TBS, Bw.David Ndibalema akizungumza katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani, kufungua mashindanoya insha na kufungua warsha ya wadau katika uandaaji wa viwango iliyofanyika leo Novemba 18,2022 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.Wadau wa uandaaji wa Viwango wakifuatilia hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani, kufungua mashindanoya insha na kufungua warsha ya wadau katika uandaaji wa viwango iliyofanyika leo Novemba 18,2022 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Wadau wa uandaaji wa Viwango wakifuatilia hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani, kufungua mashindanoya insha na kufungua warsha ya wadau katika uandaaji wa viwango iliyofanyika leo Novemba 18,2022 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akipata picha ya pamoja na wadau wa uandaaji wa Viwango katika hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani, kufungua mashindanoya insha na kufungua warsha ya wadau katika uandaaji wa viwango iliyofanyika leo Novemba 18,2022 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na wadau katika uandaaji viwango wametakiwa kuongeza juhudi katika kuoanisha viwango vyetu katika ngazi za kikanda na pia kushiriki kikamilifu katika michakato ya kutayarisha viwango vya kimataifa, ili kuziwezesha bidhaa za Tanzania kupenya kirahisi katika masoko ya kikanda na kimataifa.
Wito huo umetolewa leo Novemba 18,2022 Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akimwakilisha Waziri wa wizara hiyo kwenye hafla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani, kufungua mashindanoya insha na kufungua warsha ya wadau katika uandaaji wa viwango.
Amesema Wizara kupitia TBS huwa inatenga fedha zaidi ya shilingi milioni 150 kwa mwaka ili kuwezesha huduma kwa wajasiriamali wadogo na mapaka sasa tayari wajasiriamali takribani 500 wamepata alama ya ubora bure bila malipo yoyote.
Hatua hii imewawezesha kuzalisha bidhaa bora zenye kukidhi matakwa ya viwango hatimaye kuwawezesha kupata masoko ya kimataifa.
Aidha amesema kazi inayofanywa na TBS katika kuratibu na kusimamia utayarishaji wa viwango vya kitaifa ni kazi adhimu. Viwango husaidia si tu kufungua mipaka, lakini pia kuhakikisha usalama wa afya na mali, ulinzi wa mazingira na elimu kwa umma.
"Matumizi ya viwango husaidia kuondoa vikwazo katika biashara baina ya nchi, hivyo kusaidia kukuza uchumi wa Taifa na kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla. Viwango husaidia kusambaza teknolojia ambazo huchochea maendeleo ya uchumi wetu, hivyo kuchangia katika ustawi wa Watanzania". Amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Viwango ya kila mwaka yamelenga kuamsha uelewa miongoni mwa wadhibiti ubora, wafanyabiashara, wenye viwanda na walaji kuhusu umuhimu wa viwango kwa maendeleo ya jamii.