MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO KUHAMASISHA UTALII


Madiwani, watumishi wa Serikali, pamoja na viongozi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wakiambatana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakiangalia Vikobo katika hifadhi ya Serengeti leo. kabla ya kwenda hifadhi ya Ngorongoro.

Na Marco Maduhu, Ngorongoro

MADIWANI wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wakiambatana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, viongozi wa CCM pamoja na watumishi wa Serikali Manispaa ya Shinyanga, wametembelea hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini.



Ziara hiyo ya kutembelea hifadhi ya Ngorongoro imefanyika leo Novemba 12, 2022, wakitokea hifadhi ya Serengeti ambayo ilifanyika jana, ili kuhamasisha utalii na kuchangia pato la taifa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye ziara hiyo, amesema wameamua kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza vivutio vya utalii kwa kutembelea hifadhi hizo mbili.

“Nawaomba watanzania wajenge utamaduni wa kutembelea hifadhi zetu za utalii ili tumuunge mkono Rais wetu Samia kwa kutangaza vivutio vyetu na kukaribisha wangeni wengi kuja kuvitembelea hapa nchini na kuchangia pato la taifa,”amesema Mboneko.

Naye Diwani wa Kambarage Hassani Mwendapole, amesema tangu Rais Samia atangaze vivutio hivyo vya utalii kupitia Filamu ya The Royal Tour, ameshanghaa kuona kundi kubwa la watalii katika hifadhi hizo mbili za Serengeti na Ngorongoro wakipishana kuangalia wanyama.

Kwa upande wake mmoja wa watalii Si Ging Cong akitokea nchini China, amesema anafarijika kutembelea hifadhi za Tanzania ambazo zinawanyama wengi na wa kila aina hasa katika Mbuga ya Serengeti huku akivutiwa pia na mabonde katika hifadhi ya Ngorongoro.


Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa na watalii wa kigeni wakiangalia viboko katika hifadhi ya Serengeti leo kabla ya kwenda hifadhi ya Ngorongoro.

Uangaliaji wa vikobo ukiendelea.
Viboko wakiwa ndani ya maji.

Viboko wakiwa ndani ya maji.

Ziara katika hifadhi ya Ngorongoro ikiendelea katika Bonde la Olduvai Gorge wakisikiliza historia ya ugunduzi wa Fuvu la kichwa cha binadamu wa kwanza mwaka 1959.

Ziara katika Bonde la Olduvai Gorge ikiendelea.

Ziara katika Bonde la Olduvai Gorge ikiendelea wakiangalia mafuvu ya vichwa vya binadamu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiangalia Fuvu la kichwa cha binadamu.

Ziara ikiendelea katika Bonde la Olduvai Gorge.

Muonekano wa alivyokuwa Faru Fausta ambaye aliishi miaka 57.

 Muonekano wa alivyokuwa Faru Fausta ambaye aliishi miaka 57.

Picha ya Pamoja ikipigwa katika Makumbusho ya Bonde la Olduvai Gorge.

Picha ya Pamoja ikipigwa katika Makumbusho ya Bonde la Olduvai Gorge.

Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha zikiendelea kupigwa.
Mtalii Si Ging Cong akitokea nchini China, akielezea namna anavyofarijika kutembelea hifadhi za Tanzania.

Ziara katika Makumbusho ya Bonde la Olduvai Gorge katika hifadhi ya Ngorongoro ikiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments