TAWASANET YAWAJENGEA UWEZO WANAHABARI KUANDIKA HABARI ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA


Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo juu ya kuandika habari za sekta ya maji na usafi wa mazingira.

Na Marco Maduhu, DODOMA

TANZANIA Water and Sanitation Network (TAWASANET), wameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari, kutambua masuala yanayohusu Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira, ili wanapokuwa wakiandika habari zao waandike kwa ufasaha.

Mafunzo hayo yametolewa kwa siku mbili Jijini Dodoma kuanzia Novemba 16,2022 na yamehitimishwa Novemba 17, yakifadhiliwa na Taasisi ya Foundation For Civil Society.

Mratibu wa Mradi wa (TAWASANET) Darius Mhawi, amesema mafunzo hayo yamehusisha vyombo mbalimbali vya habari kutoka Mikoa ya Dar es Salam, Dodoma, Ruvuma, Mwanza na Shinyanga, wakiwamo wa Magazeti, Radio na Television, ambao watatumia kalamu zao kuandika habari kwa wingi zinazohusu maji na usafi wa mazingira.

“Sekta ya maji ni nyeti sana inaguza maisha ya kila siku ya mwanadamu, hivyo waandishi wa habari wakiielewa vizuri watakuwa wakiandika habari zao kwa usahihi, ikiwamo kuelimisha, kuonya na kukosoa, na hatimaye kila kitu kwenda sawa,”anasema Mhawi

Nao Waandishi hao wa habari wamesema mafunzo hayo yamewaongezea ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao katika kuandika habari za maji na usafi wa mazingira.

Mratibu wa Mradi wa (TAWASANET) Darius Mhawi, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari za Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira.

Mratibu wa Mradi wa (TAWASANET) Darius Mhawi, akiendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari za Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira.

Mwezeshaji Severine Allute akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari za Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira.

Mwezeshaji Severine Allute akiendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari za Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post