TASAC YATOA ELIMU YA ULINZI,USALAMA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MOROGORO


AFISA Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kelvin akimuonyesha mmoja wa watumiaji wa vyombo vya majini namna ya kuvaa jaketi la uokozi

Na Mwandishi Wetu,Morogoro


SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa elimu ya Usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira mkoani Morogoro pamoja na kuendesha zoezi la ukaguzi wa Vyombo vya usafiri majini.


Ukaguzi huo ni sehemu mikakati ya Shirika hilo kuhakikisha vyombo vya usafiri majini vinakuwa na ubora unaotakiwa kwa kuzingatia viwango.


Zoezi hilo liliendeshwa na Maafisa Ukaguzi na Udhibiti wa Vyombo vya Majini wa Shirika hilo, Bw. Gabriel Manase na Maulid Nsalamba katika wilaya ya Ifakara mkoani humo. Maafisa hao walitoa elimu ya usalama na ulinzi ikiwemo utunzaji wa mazingira wanapokuwa kwenye shughuli zao


Akizungumza wakati wa zoezi hilo Manase alisema elimu hiyo ina umuhimu mkubwa sana hivyo jamii inapaswa kuitambua na kuweza kuzuzungatia wakati wote wanapotekeleza shughuli zao za kila siku.


Zoezi hili lilianza tarehe 11 Novemba, 2022 ifakara katika maeneo ya Ngalimila, Ngapemba, Utengule, Chita na Mngeta na Mchombe na litaendelea katika mikoa ya iringa na Dodoma lengo ni kuhakikisha jamii inapata elimu.


Zoezi hilo liliendeshwa pia kwa ushirkiano na Afisa Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kelvin na Afisa Uhusiano Mwandamizi Amina Miruko ambapo waliitaka jamii kuhakikisha inazingatia usalama kwenye vyombo vya maji ili kuweza kuepukana na ajali ambazo zinazaweza kuwakuta wawapo safarini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments