TUME YA UTUMISHI YA MAHAKAMA IMEFANYA MKUTANO NA WADAU WA MAHAKAMA MKOA WA SHINYANGAJaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA 
 
TUME ya Utumishi ya Mahakama imefanya mkutano na wadau wa Mahakama Mkoa Shinyanga.

Mkutano huo umefanyika leo Novemba 21. 2022 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, amesema wamefanya ziara ya kukutana na wadau hao kuitangaza Tume hiyo, pamoja na kujadili uboreshaji wa utoaji haki kwa wananchi na kwa wakati.

Amesema Tume hiyo imekutana na wadau pamoja na watumishi wa Mahakama, kusikiliza maoni na kuboresha juu ya utoaji haki kwa wananchi kupitia Mahakama.

“Tume ya Utumishi wa Mahakama tumefanya ziara hapa Shinyanga, kwa lengo la kujadili uboreshaji na utoaji haki kwa wananchi, na Tarehe 25 mwezi huu tunazindua Mahakama za wilaya 18, na Kanda hii ya Shinyanga tutazindua Mahakama za wilaya ya Busega na Itilima,”amesema Prof Juma.

Naye Jaji Kiongozi na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mustapher Siyani, anasema matarajio ya Tume hiyo ni kuboresha utendaji kazi wa Mahakama, pamoja na kupunguza mrundikano wa mashauri.

Amewataka pia mawakili wasomi, wanasheria wawe wanawashauri wateja wao wafanye usuluhishi juu ya kesi zao, na siyo kila kesi ipelekwe mahakamani ili kupunguza mrundikano wa mashauri na kutopoteza muda.

“Mrundikano wa Mashauri uliopo Mahakamani hadi sasa kuanzia Mahakama za Mwanzo, Wilaya, hadi Mahakama kuu ni 3,419,”amesema Siyani.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma, amesema ziara hiyo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama utaboresha utendaji kazi wa mahakama pamoja na utoaji haki kwa wananchi na kwa wakati.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama akizungumza kwenye mkutano huo.

Jaji Kiongozi na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mustapher Siyani, akizungumza kwenye mkutano huo.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post