MTOTO WA MIAKA MITANO ASHAMBULIWA NA CHATU AKIOGELEA BWAWANI

Mvulana mwenye umri wa miaka mitano raia wa Australia amenusurika kifo baada ya kuumwa na chatu ambaye ppia alimburuta hadi kwenye bwawa la kuogelea.

Chatu huyo alikuwa na ukubwa wa takriban mara tatu ya umbo  la kijana huyo.

Kwa mujibu wa baba yake mzazi Kijana Beau Blake alikuwa akifurahia kuogelea nyumbani  kwao wakati chatu huyo mwenye urefu wa mita 3  sawa na futi 10 alipomvamia.  

Lakini Beau yuko katika hali nzuri na kwamba anaendelea vyema ingawa ana majeraha madogo tu.

Tukio hilo limeendelea kuzungumziwa katika eneo analoishi kijana huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post