DONALD TRUMP ATANGAZA KUGOMBEA URAIS MAREKANI


Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump.

Wakati kura zikiwa hazijamalizika kuhesabiwa za uchaguzi wa bunge wa katikati ya muhula wa Marekani wa 2022, rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump ametangaza nia ya kugombea urais kwa mara nyingine kupitia chama cha Republikan katika uchaguzi wa 2024.

Hii itakuwa ni mara yake ya tatu kuwania, baada kumshinda mgombea wa Demokrat, Hilary Clinton mwaka 2016, na aliposhindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi wa 2020.


Akiwa katika makazi yake ya Mar-a-Largo, Trump ametoa tangazo hilo huku wachambuzi wakiona ni kama kupuuzia madai ya Waripublikan kwamba ni yeye aliyechangia kukosekana kwa wapiga kura wengi.

Mpaka sasa bado analalamika kwamba uchaguzi uliopita alifanyiwa hila zilizo muwezesha rais wa sasa wa 46, Joe Biden kushinda.


Hata hivyo anakabiliwa na hali ngumu ya kisiasa licha ya kwamba kasi yake inaonekana kutozingatia hilo.

Trump ametoa tangazo hilo akiwa na wasaidizi wake kisiasa pamoja na wafuasi wake katika makazi yake ya Mar-a-Largo yaliyopo katika jimbo la kusini la Florida, ambayo amekuwa akiishi toka alipo ondoka madarakani mjini Washington, Januari mwaka jana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post