RC MJEMA ATAKA WAMILIKI WA MIGODI NA MAKAMPUNI SHINYANGA KUTOA MIKATABA YA AJIRA KWA WAFANYAKAZI KUEPUKA MIGOGORO

 

Na Michael Utouh- Shinyanga

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ametoa wito kwa wamiliki wa  migodi  na makampuni  mkoa wa Shinyanga kutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi ili kuepuka migogoro.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ametoa wito huo Novemba 4,2022 wakati aliposhiriki katika zoezi la utiaji saini wa mkataba wa hali bora ya wafanyakazi baina ya chama cha wafanyakaz wa migodini( TAMICO) katika mgodi wa uchimbaji madini  ya Almasi wa Williamson Diamond limited uliopo eneo la Mwadui wilaya ya Kishapu.


Ambapo amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na sekta ya uzalishaji na uchimbaji madini hapa nchini hususani kwa mkoa wa Shinyanga na mikoa yote inayohusika na uchimbaji madini hivyo kwa wachimbaji wote na wamiliki wa migodi wanapaswa kutembea kifua mbele kwa namna ambavyo serikali hii inavyowajali


Aidha Mhe. Mjema ameendelea kwa kusema mikataba ya ajira kwa wafanyakaz ni muhimu kwani kumekuwa kukitokea migogoro mbalimbali ambayo mara nyingi chanzo chake ni kutokana na kutokuwepo kwa mikataba ya ajira baina ya mwajiri na mwajiriwa hivyo kuisababisha serikali kuwa na mirundikano mikubwa ya migogoro baina ya waajiri na wafanyakaz wao


Ameongeza kwa kuwaasa wafanyakaz wote wa mgodi huo wa Williamson Diamond kuheshimu matakwa yote ya kimkataba yaliyowekwa  sambamba na kutoa wito kwa uongozi wote wa mgodi na migodi yote ndani ya mkoa kuhakikisha wanashughilikia swala la mikataba kwa wafanyakaz, kuhakikisha pia mkataba huo ambao siku ya leo wametiliana saini wanaufikisha kwa kamishna wa kazi ili uanze kazi mara moja


Mhe.Mjema amewaasa wafanyakaz wote wanaofanya kazi katika sekta ya uchimbaji madini pamoja na makampuni balimbali ambayo tayar yamewapa mikataba ya ajira wafanyakaz wake kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kuwa na moyo wa kujituma ili kuongeza ufanisi zaidi katika uzalishaji ili kuboresha maslahi yao


Kwa upande wake Meneja mkuu wa mgodi wa Wiliamson Diamond Limited Mhandisi Ayoub Mwenda amesema kuwa alikutana na wafanyakazi na kusikiliza kero zao ambao waliomba ikiwemo kupata mikopo kupitia Benki kuboreshewa mikataba ya kazi kwa waliokuwa na mikataba ya muda mfupi na kuboreshewa maslahi yao.


Amesema kuwa tayari wafanyakazi wameshaanza mikopo na zaidi ya asilimia 75 ya wafanyakazi waliokuwa na mikataba maalumu imefanyiwa kazi.


Mhandisi Mwenda amesisitiza kuwa ili kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi mgodini hapo ni wajibu kwao kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji ambao utawezesha kuboresha maisha yao, kuchangia jamii innayozunguuka mgodi huo na kuchangia katika uchumi wa Taifa.


Naye katibu mkuu wa TAMICO Peternus Rwechungula Amemshukuru Meneja Mkuu kwa kushirikiana na wafanyakazi na kusaini mkataba huo kwani ni takwa la kisheria na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana na kampuni hiyo ikiwemo kufanya majadiliano na kuboresha zaidi mkataba huo.


Pia amewahimiza wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi ili kuweza kupata haki zao, kutambuana na kujadiliana ili kuweza kupata haki zao.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post